Miongoni mwa maandalizi yanayo endelea katika mwezi wa Muharam, kitengo cha utunzaji wa haram cha Atabatu Abbasiyya kimetandika zulia jekundu katika ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) katika eneo lenye ukubwa wa mita (2500), likitanguliwa na nailoni chini yake.
Zulia hilo limeenea eneo lote la ukumbi huo mtukufu pamoja na katika milango inayo ingia kwenye haram, hii ni kwa ajili ya kulinda mazulia yaliyotandikwa katika haram na kuwarahisishia utembeaji watu wanaokuja kufanya ziara ambao idadi yao inaongezeka kila siku.
Kumbuka kua kitengo cha utunzaji wa haram ni sawa na vitengo vingine vya Atabatu Abbasiyya tukufu, wanafanya kila wawezalo katika kuweka mazingira mazuri ya kuwapokea watu wanaokuja kufanya ziara na mawaakib (vikundi) vya Husseiniyya wanao ongezeka kila siku, ambao kilele chake itakua siku ya mwezi kumi Muharam ambayo mamilioni ya watu wanatarajiwa kufanya ziara, watumishi wa vitengo vyote vya Ataba wanafanya kazi kwa bidii kuhakikisha wanatoa huduma bora zaidi kwa mazuwaru watukufu na wameongezewa wasaidizi wa kujitolea.