Kana kwamba kuta za haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) zinaita Yaa Hussein, Yaa Abbasi, Yaa Zainab..

Maoni katika picha
Kila kitu kimemlilia Imamu Hussein (a.s), inaonyesha kumlilia Imamu Hussein (a.s) hakuhusiani na binadamu peke yao, hili limethibitishwa na Qur’an tukufu pamoja na hadithi, riwaya na historia ikiwemo na uhalisia wa mazingira.

Kutoka kwa imamu Swaadiq (a.s) anasema: “Hakika Abu-Abdillahi (a.s) wakati alipo uawa, zilimlilia mbingu saba na aridhi saba na vyote vilivyomo ndani yake na baina yake, na viumbe wote waliopo peponi na motoni, na kila kinacho onekana na kisicho onekana”.

Ibun Mandhuur, katika kitabu cha Muhtasar wa historia ya Damaska ameandika kua: “Siku aliyo uawa Hussein..(a.s) hakuna jiwe lolote lililo inuliwa ispokua chini yake zilikutwa damu”.

Riwaya kama hii zipo nyingi sana, hazina ukomo, zote zinasisitiza kitu kimoja, kinacho maanisha kua imamu Hussein (a.s), ana nafasi kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu mtukufu, na anakarama nyingi sana, sio jambo geni kuliliwa na ulimwengu na kila kilichomo, sasa itakuaje kwa jiwe lililo tumika kujenga ukuta wa kaburi la mtu ambaye Imamu Hussein (a.s) baada ya kuuawa kwake kishahidi alisema (Hivi sasa umevunjika mgongo wangu).

Anaye kusudia kutembelea malalo ya mbeba bendera ya Imamu Hussein (a.s) na kamanda wa jeshi lake, ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) katika siku hizi, kana kwamba anakumbuka maneno hayo na anaishi katika mazingira hayo, popote atakapo angalia ndani ya uwanja wa haram tukufu, ataona mazingira ya Ashura yamemzunguka, muonekano wa huzuni za Ashura ulio tengenezwa na idara ya ushonaji ya Atabatu Abbasiyya tukufu, walio chukua jukumu la kuvisha nguo nyeusi zilizo dariziwa maandishi yenye ujumbe mbalimbali (Yaa Hussein, Yaa Abbasi, Yaa Zainab) majina hayo matatu yamepamba ukumbi mtukufu wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kutokana na utukufu wao tumeangaziwa utukufu wa milele.

Jengo la Atabatu Abbasiyya tukufu limevishwa vazi jeusi, vitambaa vyote vimedariziwa maneno yanayo ashiria huzuni za Ashura, pamoja na beti za kimashairi na maneno aliyo sema Abulfadhil Abbasi (a.s) katika vita ya Twafu ya milele, na maneno ya maimamu (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: