Mawakibu (vikundi) vya maombolezo ya Ashura vyakumbuka kuwasiri kwa Imamu Hussein (a.s) katika aridhi ya Karbala, mbele ya Ataba mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya)..

Maoni katika picha
Inafahamika wazi kwa wapenzi wa Ahlulbait (a.s) na wafuasi wao, wanapo huisha msiba wa Abu-Abdillahi Hussein (a.s), huzigawa siku za Ashura kutokana na matukio, ili kuangazia misukosuko yote waliyo ipata watu wa nyuma ya Mtume (a.s), ikiwa ni pamoja na tukio la siku ya pili katika mwezi wa Muharam, siku hiyo hufanyika kumbukumbu maalumu ya kuwasili kwa Imamu Hussein (a.s) na watu wake katika aridhi ya Karbala.

Watu wa Karbala kupitia maukibu (vikundi) vyao, hukumbuka msiba huu kwa namna mbalimbali, wengine huwasha kandili, na wengine hufanya matembezi ya maomboleza, (hupiga matam na zanjiil) pamoja na majaalis (vikao) vya mawaidha na miongozo ya kidini.

Haram ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), jana mwezi pili Muharam na usiku wake zilishuhudia kuwasili kwa mawaakibu (vikundi) vingi, lakini waliingia kwa kufuata muda na ratiba iliyopangwa na kitengo cha minasabati na mawaakibu cha Ataba mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya), huku wamebeba bendera na mabango yaliyo andikwa ujumbe mbalimbali unao himiza kushikamana na misingi ya harakati na muhanga wa Imamu Hussein (a.s), ulio lenga kuondoa dhulma na kupambana na matwaghuti kwa namna yeyote ile.

Kumbuka kua mwezi wa Muharam unasampuli nyingi za kuomboleza msiba huu mkubwa, ulio mkumba Imamu Hussein (a.s) na watu wake, miongoni mwa sampuli za uombolezaji ni kuzipa uhusika maalumu siku za mwanzo, na zingine hupewa majina ya watu wa Ahlulbait (a.s) na baadhi ya majemedari wa vita ya Twafu (r.a), walio jitolea damu zao na roho zao kwa ajili ya kumnusuru Imamu Hussein (a.s). Hivyo kila siku hupewa jina la mtu au aina ya tukio, fahamu kua Imamu (a.s) na watu wa nyumbani kwake pamoja na maswahaba zake waliuawa siku ya kumi ya mwezi wa Muharam.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: