Wizara ya elimu ya juu na utafiti wa kielimu yakitunuku chuo cha Ameed uthibitisho wa mwisho..

Maoni katika picha
Wizara ya elimu ya juu na utafiti wa kielimu yakitunuku cheti cha kukitambua na kukithibitisha chuo kikuu cha Ameed, kilicho chini ya kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu na vitivo (vitengo) vyake (Udaktari, Udaktari wa meno na uuguzi), baada ya kupata ruhusa ya kuanzishwa kwake kutoka katika baraza la mawaziri namba 234 ya mwaka 2017, inayo anza kufanya kazi mwaka huu 2017-218.

Uthibitisho wa wizara wenye namba 6519 wa tarehe 19 Septemba 2017, umetolewa chini ya kanuni namba 25 ya mwaka 2016, baada ya chuo kikuu cha Ameed kukidhi vigezo vyote vilivyo wekwa na wizara.

Waziri wa elimu ya juu na utafiti wa kielimu dokta Abdurazaaq Issa alimkabidhi katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Muhandisi Muhammad Ashiqar cheti cha uthibitisho wa kupasishwa katika hafla ya uzinduzi wa chuo cha Waarithul-Ambiyaa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: