Atabatu Abbasiyya tukufu yafanya majlis za Ashura..

Maoni katika picha
Katika mazingira ya huzuni kubwa nyoyo zilizo jaa simanzi na macho yanayo bubujika machozi kutokana na msiba wa kuuawa kishahidi kwa Imamu Hussein (a.s), kama ilivyo kila mwaka, Atabatu Abbasiyya tukufu inafanya majlisi chini ya kitengo cha utumishi ndani ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kuhuisha kumbukumbu ya kuuawa kwa Imamu Hussein (a.s) pamoja na watu wa nyumbani kwake na maswahaba wake.

Rais wa kitengo cha utumishi cha Atabatu Abbasiyya tukufu Haji Khaliil Hanuun amesema kua: “Majlisi hizi hufanywa kila mwaka, na hudumu siku kumi na tatu, kuanzia Muharam mosi, mara mbili kila siku, Asubuhi na baada ya dhuhurain (mchana), haziingiliani na vikundi vya maombolezo vinavyo ingia katika haram tukufu, na hupata mahudhurio makubwa kutoka kwa watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) na watu wanaokuja kufanya ziara”.

Akasema kua: “Tulikubaliana na kitengo cha dini cha Atabatu Abbasiyya kiandae wahadhiri watakao zungumza kila siku maswala ya Fiqhi na Aqida pamoja na mambo yanayo husu harakati ya Imamu Hussein (a.s) na vipi amekua taa linalo angazia watu huru kote duniani pamoja na kutofautiana tamaduni na mielekeo yao, hakika amekua ni muongozo kwa watu wote bila kujali ukabila wala utaifa”.

Hanuun akabainisha kua: “Majlis huhitimishwa kwa matam ambayo huongozwa na mwimbaji Mula Hamid Tamimi, ambaye huimba Qaswida za kimashairi zinazo elezea yaliyo mkuta Imamu Hussein (a.s) na watu wake katika siku kama hizi”.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu hufanya majlisi zinazo lenga kufafanua maswala ya kifiqhi na kiaqida pamoja na kuelezea dhulma walizo fanyiwa Ahlulbait (a.s) kwa ujumla, hali kadhalika kufafanua malengo ya muhanga mtukufu wa Imamu Hussein (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: