Kwa picha: Mawakibu za Karbala zakumbuka ujasiri wa Muslim bun Aqiil (a.s)..

Maoni katika picha
Wanahistoria wameandika ushujaa wa Muslim… Kasifiwa kwa ujasiriri ulio washa vita ya kutetea uadilifi… Kutokana na uadilifu wake alipandisha bendera ya kuthibitisha ujumbe wake… Na upanga wake ulitikisa mji wa Kufa, ulitetemesha Qasri la utawala, ewe Muslim kwa ujasiri wako.

Maneno haya na mengineyo yalisikika katika mawakibu (vikundi) vya maombolezo ya Ashura katika usiku wa nne wa mwezi wa Muharam, wakiwa katika malalo ya imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), walikua wakikumbuka ushujaa na ujasiri wa Muslim bun Aqiil (a.s), katika kupambana na matwaghuti wa bany Umayya, na kuuawa kwake kishahidi katika siku ya tisa ya mwezi wa Dhulhijjah mwaka wa 60 hijiriyya.

Pamoja na kuuawa kwake kishahidi mwezi tisa Dhulhijjah, lakini imekua ni desturi ya waombolezaji wa Ashura kwa vizazi na vizazi kutenga siku maalumu ya kumkumbuka mtu huyu jasiri, kama sehemu ya kumuenzi, hakika anastahiki zaidi kuenziwa, alijitolea nafsi yake kwa ajili ya kuinusuru dini, akawa mtu wa kwanza kuuawa katika harakati ya Imamu Hussein (a.s), taarifa ya kuuawa kwake ilipo fika kwa Imamu (a.s), alilia na akasema: Mwenyezi Mungu amrehemu Muslim, amekua kipenzi wake na yupo chini ya radhi zake, ametekeleza wajibu wake bado nasisi tutekeleze wajibu wetu.

Kumbuka kua mwezi mtukufu wa Muharam kuna aina nyingi za maombolezo ya msiba mkubwa aliopata Imamu Hussein na watu wa nyumba ya Mtume (a.s), miongoni mwa desturi za uombolezaji ni kuzipa siku za kwanza majina ya watu wa nyumba ya Mtume (a.s) na maswahaba wa Imamu Hussein waliokua na mchango mkubwa katika vita ya Twafu (Karbala), hivyo kila siku hupewa jina la mtu au jambo kubwa lililo tokea katika siku kama hiyo, fahamu kua Imamu na watu wa nyumbani kwake waliuawa siku ya mwezi kumi Muharam.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: