Miongoni mwa majemedari wa Twafu ni Huru Riyahi (r.a)..

Maoni katika picha
Miongoni mwa mashahidi watukufu wa Ashura, na miongoni mwa watu wema walio jitolea nafsi zao kwa ajili ya kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu na kumnusuru Imamu Hussein (a.s) ni Huru bun Yazidi bun Najiya bun Qa’anab bun Ataab bun Harami bun Riyahi, katika bani Tamim, Huru alikua mtu maarufu kwa waarabu, na shujaa wa waislamu, na alikua ni kamanda wa bani Tamim, kiongozi wa Kufa Ubaidullahi bun Ziyadi alimtuma Huru kwenda kumzuia Imamu Hussein (a.s) kuingia katika mji wa Kufa akiwa na wanajeshi elfu moja.

Akaondoka na jeshi lake kwenda kutekeleza agizo hilo, akakutana na msafara wa Imamu Hussein (a.s) katika sehemu iitwayo Dhihasmi, akaanza kufuatana na msafara wa Imamu Hussein hadi wakafika katika aridhi ya Karbala, aliendelea kua pamoja nao hadi mwezi kumi Muharam, alipo ona jeshi la bani Umayya limekusudia kumshambulia Imamu Hussein (a.s), akaanza kutafakari upya swala hilo, akatembea kuelekea kwa Imamu Hussein (a.s) kidogo kidogo huki anatetemeka, baadhi ya watu wake wakamuuliza kwa nini anatetemeka na anaonekana kua mnyonge sana, akawajibu kua: “Wallahi mimi nahiyarisha nafsi yangu baina ya pepo na moto, wala sioni kama naweza kupata pepo japo kidogo, hata kama nikikatwakatwa na kuchomwa”, akaondoka na farasi wake hadi kwa Imamu Hussein (a.s), alipo fika kwa Imamu (a.s) akamuuliza, Je! Naweka kukubaliwa toba yangu? Imamu akamjibu: “Ndio, Mwenyezi Mungu atakubali toba yako na atakusamehe”.

Huru akakaa mstari wa mbele wa wapiganaji wa Imamu Hussein (a.s), akaanza kuhutubia jeshi la maadui, akawaambia kua: “Enyi watu hivi hamumkubalii Imamu Hussein (a.s) hata jambo moja miongoni mwa mambo mengi aliyo kuambieni!!? Mwenyezi Mungu akusameheni na muache kumpiga vita na kumuua? Nakulinganieni, hakika huyu ni mtu mwema, amekujieni mnamtupa, na kudai kua mnapigana kuokoa nafsi zenu kutokana na yeye na mmejiandaa kumuua, mme mkamata na kumbugudhi, mnamzuia kwenda maeneo mengine, amekua sawa na mateka mikononi mwenu, mmemsumbua yeye, wanawake, watoto na wafuasi wake, mmewazui kunywa maji ya mto Furat, Mwenyezi Mungu hatakupeni maji siku yenye kiu kali msipo tubia makossa yenu”.

Kuuawa kwake kishahidi:

Huru aliomba ruhusa kwa Imamu Hussein (a.s) ya kwenda kupigana, Imamu akamruhusu, akaingia katika uwanja wa vita kupambana na jeshi lililokua likiongozwa na Omari bun Saadi huku akisema:

Mimi ndio Huru mafikio ya wageni** Nitakushambulieni kwa jambia.

Kwa ajili ya kumtetea mbora wa waliopita katika miji ya Khaifu**

Nakushambulieni wala sioni yeyote kutoka Haifu.

Akaanza kuwafyeka kwa jambia leke, akaua zaidi ya maadui arubaini, ndipo wakajikusanya na wakamzunguka wakafanikiwa kumzidi nguvu, na walio ongoza mapambano yaliyo mmaliza nguvu ni Ayubu bun Masrahu na mtu mwingine kutoka katika mashujaa wa mji wa Kufa, watu wa Imamu Hussein (a.s) wakaja kumuokoa Huru katikati ya maadui akiwa hajiwezi kabisa, wakambeba na kumpeleka kwa Imamu Hussein (a.s), Imamu akawa anamfuta fumbi usoni kwake huku anamuambia: “Wewe ni Huru kama alivyo kwita mama yako, umekua huru hapa duniani na utakua mtukufu kesho akhera”. Hapo akakata roha na akawa amefariki mwaka wa 61 hijiriyya katika vita ya Karbala.

Kaburi la Huru lipo umbali wa Farsakh moja kutoka mji mtukufu wa Karbala, hadi leo watu huenda kumzuru huko, hatujui sababu zilizo pelekea azikwe sehemu hiyo, inasemekana watu wake ndio walio mtoa sehemu ya vita na kwenda kumzikia huko.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: