Miongoni mwa majemedari wa Twafu: Habibu bun Mudhahir Al-Asadiy (r.a)..

Maoni katika picha
Maswahaba wa Imam Hussein (a.s) wanasifa za pekee zinazo wafanya kua mashahidi bora zaidi, watu hao walikua na mawasiliano maalum na imamu wao wa zama Abuu Abdillahi Hussein (a.s), walikua na mshikamano bora, uliokidhi matakwa ya sheria, ya kumtambua na kumtii imamu wa zama zao, miongoni mwa watu hao watukufu ni Habibu bun Mudhahir Al-Asadiy, alikua ni miongoni mwa maswahaba wa Mtume (s.a.w.w), na alikua anaishi katika mji wa Kufa, pia alikua ni mfuasi wa kiongozi wa waumini Ali bun Abutwalib (a.s) wakati wa ukhalifa wake na alipigana pamoja naye katika vita zote.

Habibu alikua mtu maarufu katika mji wa Kufa, na nimiongoni mwa watu walio muandikia Imam Hussein (a.s) barua za kumuomba aje katika mji wa Kufa.

Alipo wasili Muslim katika mji wa Kufa na akafikia katika nyumba ya Mukhtari, wafuasi wa Imam Hussein (a.s), walimzunguka na Habibu bun Mudhahir alikua miongoni mwa watu walio eleza wazi mapenzi yao kwa Imam Hussein (a.s).

Habibu na Muslim bun Ausaja walishiriki katika kuchukua viapo vya utii wa Imam Hussein (a.s) kwa watu wa Kufa, alipo wasili ibun Ziyadi katika mji wa Kufa na akawafarakanisha watu na balozi wa Imam (a.s), walijificha na baadae wakaungana na Imam Hussein (a.s).

Habibu alipo ona uchache wa wafuasi wa Imam Hussein (a.s) walio kuwepo Karbala, aliomba ruhusa kwa Imam (a.s) ili aende kwa watu wake Baniy Asadi akawaambie waje kumnusuru, Imam akamruhusu, Habibu akaenda na akaongea na watu wake, wapo waliokubali kwenda kumnusuru Imam, lakini majasusi wa Omari bun Saadi walifanikiwa kujipenyeza na kuwashawishi wasiende na wakaweza kusababisha ubishi baina yao na mwisho hawakwenda, akarudi pekeyake Habibu bun Mudhahir kwa Imam Hussein (a.s) na akamuelezea yaliyo jiri.

Siku ya Ashura Habibu alipewa uongozi wa kikosi cha jeshi la Imam (a.s), alikua upande wa kulia wa Zuhair bun Qain.

Alipo anguka chini rafiki yake wa muda mrefu Muslim bun Ausaja, Habibu na Imam walimfuata na wakasimama mbele ya kichwa chake, Habibu akasema: “Msiba wako umekua mkubwa sana kwangu ewe Muslim, nakubashiria pepo”

Muslim akamuambia huku akiashiria kwa Imam (a.s): Mwenyezi Mungu akupe bishara njema… mimi nakuusia kuhusu huyu, pigana kwa ajili yake hadi ufe.

Habibu akasema: Naapa kwa Mola wa Kaaba, nitatekeleza.

Abuu Abdillahi Hussein (a.s) alipo omba apewe muda wa kutekeleza ibada ya swala ya Adhuhuri, Haswin bun Tamim, aliye kua upande wa jeshi la maadui alisema kua, haikubaliki.

Habibu hakusikiliza upuuzi huo, akamuambia: “Unadai haikubaliki swala kwa watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w), na inakubalika kwako”. Haswin akamvamia, Habibu akaingia katika uwanja wa vita, akapigana vita kali sana, akaua mtu katika bani Tamim aitwaye Badil bun Swarim, mtu mwingine katika bani Tamim akamchoma mkuki Habibu akaanguka chini, alipo taka kuinuka Haswin akampiga panga la kichwani, akaanguka chini na akakata roho. Wengine wanasema Badil bun Swarim ndiye aliye muua Habibu bun Mudhahir.

Baada ya kufariki kwa Habibu bun Mudhahir Imam Hussein (a.s) alihuzunika sana, kutokana na nafasi aliyo kua nayo kwake, Imam akasema: “Nafsi yangu na za wenye kuwahami maswahaba wangu nazielekeza kwa Mwenyezi Mungu”.

Siku anafariki alikua na umri wa miaka sabini na tano.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: