Miongoni mwa majemedari wa Twafu ni Muslim bun Ausaja

Maoni katika picha
Miongoni mwa watu maarufu katika mji wa Kufa ni Muslim bun Ausaja bun Thaalaba Al-Asadiy (r.a), alijulikana kwa uchamungu na utukufu, alikua na heshima kubwa, ni swahaba, alimuona mtume na akapokea hadithi kutoka kwake, pia ni miongoni mwa waliomuandikia Imam Hussein (a.s) barua za kumwita katika mji wa Kufa.

Ndiye aliye muambia Imam Hussein (a.s) kua “Hivi sisi tunaweza kujitenga na wewe? Tutamuambia nini Mwenyezi Mungu, wallahi sitapumzika hadi niwashambulie kwa mshale wangu na kuwapiga kwa panga langu, sitakuacha hata kama nikiwa sina siraha, nitawapika kwa mawe hadi nife pamoja na wewe”

Alizingatia ahadi yake na akathibitisha maneno yake, ushujaa wake ulionekana katika viwanja vya Twafu, historia imetunza mashairi yake aliyo sema wakati anaingia katika uwanja wa vita:

Mkiuliza kuhusu mimi mjue mimi ni Dhuu labad* hakika nyumba yangu ipo kwa baniy Asad.

Atakaye nifanyia uadui yupo nje ya rushd* na ni kafiri wa dini ya Jabbaaru Swamad.

Imam Hussein (a.s) na Habibu bun Mudhahir walimkimbilia baada ya kuanguka chini akiwa katika mapambano makali siku ya Ashura huko Karbala, wakamkuta bado hajafariki, ukiwa uso wake umejaa damu na nguvu zimemuisha, Imam Hussein (a.s) akamsogelea na akamuambui, Mwenyezi Mungu akurehemu ewe Muslim, na akasoma aya isemayo (…Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo).

Kisha Habibu akamsogelea na akamnong’oneza sikioni “Msiba wako umekua mkubwa sana kwangu ewe Muslim, nakubashiria pepo”

Muslim akasema kwa sauti ya chini “Nakubashiria heri ya pepo”.

Habibu akahitaji kupewa usia zaidi na Muslim, akamuambia kama si kua upo katika hali mbaya ningependa unihusie chochote unacho taka, Muslim akasema: “Nakuhusia kuhusu huyu –akamuashiria Imam Hussein- ufe kwa ajili yake”.

Kisha Muslim akafariki mbele ya Imam Hussein (a.s) na Habibu bun Mudhahir (r.a), kijakazi wake akapiga kelele akisema: Waa Muslimaahu, Yaa bun Ausajaahu, Yaa Sayyidaahu.

Wapambe wa Amru bun Hajaaj –wapiganaji wa jeshi la adui- wakaanza kusema: Tume muua Muslim bun Ausaja.

Shabthu bun Rabii alipo wasikia, akawaambia: “Ole wenu! Mnamuua mtu kama Muslim na mnafurahi? Yawezekana yeye ndiye aliyekua na msimamo bora kuliko watu wengine”. Alikua amesha ua watu sita katika maadui kabla ya kuzidiwa nguvu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: