Ujumbe wa Twafu: (Ujumbe kwa Answaar).

Maoni katika picha
Salam ewe mto wa maazimio na matashi, ni imani iliyoje iliyo kufanyeni muweze kusimama mbele ya jabali la ukafiri Yazidi na vibaraka wake, mkiwa wachache mkaendelea kua majasiri pamoja na uchache wenu. Naam, wallahi maamuzi yenu ya jana yamejaa katika historia, hakika mtakumbukwa milele, lakini historia imehusudu mbele yenu, naona uso wake unatoka jasho kuujaza mto wa Furat mlio nyimwa kunya maji yake, haukushuhudiwa kabla yenu wala baada yenu msimamo wa watu utakao linganishwa na msimamo wenu, pale mlipo simama pamoja na Imam Hussein (a.s) huku mkijua wazi kua mtauawa.

Natuma salamu kwenu vijana mliopo katika uwanja wa vita, na wale waliopo katika vikundi vya maombolezo ya Ashura, mnasifika kwa misimamo yenu mizuri, wallahi hamjazembea wala kunyongea na nyie ni kigezo kizuri, mmembeba Hussein (a.s) katika nyoyo zenu, na inapita damu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) katika mishipa yenu.

Kwenu natuma salamu zao, nao wanaendelea na ushindi katika kukomboa aridhi tukufu ya Iraq, kipande cha aridhi baada ya kingine, wanajitolea kama mlivyo jitolea, wakiinusuru aqida yao, hii ndio njia ya kujitolea kwenu ambako watu watafuata njia hiyo katika kila zama, wanapambana na kila muovu atakaye taka kuichafua dini ya Mtume wetu mtukufu (s.a.w.w), alisema kuhusu nyie Imam Husein (a.s) “Amma baad: Hakika mimi sifahamu maswahaba waaminifu zaidi wala maswahaba bora kuliko maswahaba wangu…” mlisema “Hakuna maisha bora baada yako ewe Abuu Abdillahi Hussein”. Hakika hakuna maisha mazuri baada ya kumwagika damu zenu enyi Answaar wa Hussein (a.s), kutokana na jihadi yenu mmeandika historia ya umma wa kiislamu, pongezi nyingi ziwe kwenu enyi majemedali mliojaza utukufu katika umma wa kiislamu na kuleta utukufu na heshima ya dini kwa damu zenu takatifu, na mmepandisha juu bendera ya Hussein, amani ya Mwenyezi Mungu iwe nanyi, pamoja na wapambanaji waliokua pamoja na Imam Hussein (a.s) na wapiganaji wa zama zetu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: