Kwa nini mwezi saba Muharam, imekua siku maalum kwa ajili ya Abulfadhil Abbasi (a.s)?

Maoni katika picha
Hakika siku kumi za kwanza katika mwezi wa Muharam, -kama tulivyo tangulia kusema huko nyuma- zimepewa majina ya watu waliokua na mchango mkubwa katika kumnusuru Abuu Abdlillahi Hussein (a.s) katika tukio la Twafu, historia imeandika matukio yao kwa wino wa nuru, wamekua ni mfano bora zaidi na wamepata utukufu mkubwa, majina yao yatakumbukwa vizazi na vizazi.

Miongoni mwa matukio muhimu ni lile la mbeba bendera ya Imam Hussein (a.s) Abulfadhil Abbasi (a.s), tukio lenye somo na mazingatio makubwa, tukio linalo onyesha kilele cha kujitolea.

Kutokana na umuhimu wa tukio hilo, ilichaguliwa siku ya saba kua siku maalum ya kumzungumzia kamanda huyu mtukugu, wahadhiri na waimba qaswia pamoja na vikundi vyote vya waombolezaji wazungumzie ushujaa, ujasiri na moyo wa kujitolea kwa Abulfadhil Abbasi (a.s), kwa ajili ya ndugu yake Imam Hussein (a.s), na kuacha kwake kunywa maji akiwa katika mto wa Alqamiy (Furat) huku anakiu kali, kwa kukumbuka kwake kiu ya ndugu yake Hussein (a.s), hili ni tukio kubwa ambalo hukumbukwa kila mwaka katika vikao vya maombolezo.

Kuchaguliwa kwa mwezi saba Muharam, kua siku maalumu ya kumzungumzia Abulfadhil Abbasi (a.s), kunatokana na riwaya isemayo kua; mwezi saba Muharam Abulafadhil Abbasi (a.s) baada ya kusikia watoto na watu wa nyumba ya mtume wanalia kiu imewashika na hawana maji. Alienda kuchota maji kwa nguvu na kuwaletea, alienda akiwa na wapanda farasi thelathini, pamoja na watembea kwa miguu ishirini, wakiwa na viriba (vyombo) vya kuchotea maji ishirini, wote kwa pamoja wakavamia mto wa Furat, wakitanguliwa na Naafii bun Hilali Almuradi, wakamshinda nguvu Amru bun Hajjaaj Zubaidi bamoja na wapiganaji wake walio pewa jukumu la kulinda mto.

Majemedari kutoka upande wa Imam Hussein (a.s), walivamia mto na kujaza maji katika viriba (vyombo) vyao, Amru bun Hajjaaj akiwa na wapiganaji wake wakataka kuwazuia, ndipo wakapigana vita kali sana ikiongozwa na Abulfadhil Abbasi (a.s) pamoja na Naafii bun Hilali, vita ilikua kali lakini hakuna aliye fariki pande zote mbili, maswahaba wa Imam Hussein (a.s) wakarudi salama na maji yao chini ya uongozi wa Abulfadhil Abbasi (a.s).

Imepokewa kua Abulfadhil (a.s) ni mnyesheji maji wa watu wa Imam Hussein (a.s), na ndiye aliye waokoa katika kiu kali, kuanzia siku hiyo akapewa jina la sifa (laqabu) ya Mnyweshaji wa maji, na hilo ndio jina mashuhuri zaidi kwake, watu wengi wanamjua kwa jina hilo, nalo ni jina tukufu zaidi kwake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: