Ujumbe wa Twafu: Kwa Sayyid Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Umefika wakati wa Ashura, masikio ya roho yamejaa visomo vya upendo, na moshi wa mahema unapanda katika moyo, na mawingu angani yanashusha mvua kwenye majeraha yako ewe mwana wangu, nafsi inayo kutambua inagaragara aridhini kwa utukufu wako, miguu inatembea kuja kwako, sikuona maji ispokua nilikukumbuka wewe, vipi ule mkuki uliweza kupiga katika kichwa chako kitukufu, na wewe ni mtoto wa kiongozi wa waumini (a.s) na ndugu wa wajukuu wawili wa Mtume (a.s)? ulikua na nini ule mshale uliochoma jicho lako? Haukuona nuru ya uso wako iangazayo ewe mwezi ung’aae?

Nakuandikia ushuhuda uliokufanya udumu milele na milele kwa mambo uliyo yafanya katika siku kama ya leo, ulipo wasambaratisha wanajeshi waliokua wanalinda mto, wewe pekeyako ukawa kwao kana kwamba unawazidi kwa idadi, ukawanywesha maji matam waliokua mahemani, wallahi ukawa ni mnyweshaji maji wa watu wenye kiu (Saaqi atwaasha), ewe mwana wa kiongozi wa waumini, sote leo tunakiu na wewe, hatuna uwezo wa kuvumilia tukio hili, baada yako mishale elfu imeshambulia hema la uislam, na wakina Yazidi elfu wanafanya uadui wao katika hema za Iraq, hakuna wa kupambana nao zaidi ya jeshi lako ewe bwana wangu?

Natuma katika kaburi lako ewe kibla ya watekelezaji wa ahadi, ewe mbeba bendera ya Husseiniyya, salamu zikufikie zilizojaa amani na imani, aridhi haijaleta mtu wa mfano wako ewe bwana wangu, dua yangu kwa Mwenyezi Mungu kwako, uwashufaie walio jitolea damu zao kua ngao, hao ndio walio kubeba wakakuweka katika nyoyo zao, wamejitolea kua wapiganaji kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, wamejitolea kulinda kila ncha ya aridhi ambayo wafuasi wa baniy Umayya makafiri wanataka kuichafua, na kurudisha aliyo yafanya Yazidi katika zama zake.

Ewe bwana wangu! Nakutumia salamu za waombolezaji miongoni mwa wafuasi wako, wanaokumbuka matukio ya Ashura, na salamu za wale ambao hawakuweza kufika katika kaburi lako takatifu, nakudondosha machozi yao katika kaburi lako kumpa pole Ummul-Banina, ewe bwana wangu, kupitia wewe natuma rambirambi za msiba wa ndugu yako Hussein (a.s), Mwenyezi Mungu akuze malipo yetu kutokana na utukufu wenu enyi viongozi watukufu wa dunia.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: