Atabatu Abbasiyya tukufu yaongeza ulinzi na kuboresha huduma kwa watu wanaokuja kufanya ziara katika siku za Ashura..

Maoni katika picha
Kutokana na kukaribia kidogo kidoga siku ya tukio kubwa la kuuawa kishahidi kwa Imam Hussein (a.s), Atabatu Abbasiyya tukufu imeongeza ulinzi na kuboresha huduma kwa watu wanaokuja kumzuru Imam Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), wanaotoka ndani na nje ya Iraq, ziara ambayo kilele chake ni siku ya Juma Pili ijayo ambayo ndio mwezi kumi Muharam, siku inayo tarajiwa kua na mamilioni ya watu watakaofanya ziara.

Njia zote zinazo ingia katika eneo la malalo matukufu zimekua na misururu mikubwa ya watu, na idadi inaendelea kuongezeka, pia vikundi vya kutoa huduma (mawaakib) zimeenea kila sehemu, wote wanasukumwa na mapenzi ya Ahlulbait (a.s), na wanaonyesha kuthamini mchango wao wa pekee katika kulinda imani hii tukufu, na kuweka misingi ya kupambana na uovu na utwaghuti.

Watumishi wa vitengo vyote vya Atabatu Abbasiyya tukufu wakishirikiana na wale wa kujitolea wameimarisha ulinzi na kuboresha huduma, kwa ajili ya kuhakikisha watu wanafanya ziara kwa amani na utulivu, bila kutokea jambo lolote litakalo wakwaza na kuharibu utulivu wa kiroho walio nao, pamoja na mazingira mazuri yaliyopo katika Ataba mbli (Husseiniyya na Abbasiyya) tukufu, wanatoa huduma bora kwa mamilioni ya mazuwaru kutoka ndani na nje ya Iraq.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu ilikua imesha weka ulinzi mkali na imeboresha utoaji wa huduma kwa watu wanaokuja kufanya ziara katika kipindi hiki cha maombolezo ya kifo cha Abul-Ahraar na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), wamejipanga vizuri kwa ajili ya kufanikisha zoezi hili tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: