Hivi punde: Marjaiyya yabainisha msimamo wake kuhusu kura ya kujitenga kwa kaskazini ya Iraq (Kurdistan).

Maoni katika picha
Marjaiyya imebainisha msimamo wake kuhusu kura ya kujitenga kwa kaskazini ya Iraq, imetahadharisha hatari ya kua na taifa huru upande wa kaskazini ndani ya taifa hilo, amesisitiza umuhimu wa kufuata katiba katika kutatua tatizo hilo.

Hayo yamesemwa katika hutuba ya pili ya swala ya Ijumaa ya (8 Muharam 1439h) sawa na (29 Septemba 2017m) iliyo swaliwa katika ukumbi mtukufu wa haram ya Imam Hussein (a.s), ambapo alibainisha msimamo wa Marjaiyya kuhusu kura ya kujitenga, kwa kusema kua:

“Watu wa Iraq wenye subira wanapo karibia kushinda mtihani wa magaidi wa Daesh kutokana na utukufu wa makamanda wa jeshi letu na wanao pigana pamoja nao –kwa masikitiko makubwa- unaingia mtihani mpya wa jaribio la kugawa nchi, na kukata sehemu ya kaskatizi ya nchi hii kua nchi huru, mchakato wa jambo hilo ulianza siku nyingi, pamoja na juhudi kubwa zilizo fanywa za kuwasihi ndugu zetu watukufu katika jimbo la Kurdistani wasifanye jambo hilo”.

Akaendelea kusema kua: “Marjaa dini mkuu, ambaye kwa muda mrefu amekua akisisitiza umuhimu wa umoja wa taifa la Iraq aridhi na raia wake, amefanya kila awezalo kwa ajili ya kuondoa ubaguzi na kuleta usawa kwa wairaq wa tabaka zote, anawaomba pande zote zifuate katiba ya Iraq kwa kutekeleza yaliyomo kwa moyo wote. Tofauti zinazo tokea baina ya serikali kuu na serikali ya jimbo la Kurdistani zinaweza kutatuliwa kwa njia ya amani kupitia mahakama kuu ya taifa, kama ilivyo katika katiba, na inatakiwa kufuata maamuzi ya mahakama”.

Akabainisha kua: “Hakika hatua ya kuligawa taifa na kujitenga, iwapo jambo hilo likiachwa, litakua na madhara makubwa ndani na nje ya nchi, linaweza kuleta hatari katika maisha ya ndugu zetu wapenzi wakurdi, tena inaweza kua hatari zaidi Mwenyezi Mungu atuepushe na hilo, pia kufanya hivyo kutafungua milango ya watu mbalimbali na mataifa tofauti kuja kufanya mambo kwa maslahi yao na muathirika mkuu ni raia wa nchi yetu”.

Akaongeza kua: “Hakika Marjaa na kila mwenye mapenzi na uchungu na watu wa Iraq anawaomba viongozi wa Kurdistan kuruki katika katiba na kutatua tofauti zao na serikali kuu kwa kufuata katiba”.

Wito wa Sayyid Swafi: “Serikali ya Iraq na viongozi wa kisiasa wakiwemo wabunge, wahakikishe maamuzi yao yote kuhusu ndugu zetu wakurdi yanafuata katiba”.

Akamaliza kwa kusema: “Enyi wananchi watukufu, hakika yaliyo fanywa na wanasiasa hivi karibuni, yasisababishe kukata undugu na ushirikiano wetu madhubuti uliopo kati ya muarabu, mkurdi, mturkuman na wengineo, bali inatakiwa tuonyeshe mshikamano wetu zaidi, na tujiepushe na jambo lolote linalo weza kuharibu mapenzi na undugu wa raia watukufu wa Iraq”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: