Usiku wa mwezi tisa Muharam vikundi vya Husseiniyya (mawakibu) wamkumbuka mtoto Abdullahi aliye kua ananyonya

Maoni katika picha
Miongoni mwa mambo yanayo huzunisha na kuumiza sana katika tukio la Twafu ni kuuawa kwa mtoto mdogo wa Imam Hussein (a.s) aliye kua bado ananyonya aitwae Abdallah.

Vikundi vya maombolezo (mawakibu) kama kawaida yao kwa miaka mingi wamekua wakifanya kumbukumbu hii yenye kuumiza, ndani ya malalo tukufu ya Imam Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), na kumbukumbu hii imetengewa siku ya tisa katika mwezi wa Muharam, siku hiyo hufanywa maombolezo maalumu ya kumpa pole Imam Hussein (a.s) kufuatia kuuawa kwa mtoto wake mchanga, hushiriki watoto wadogo walio vaa nguo za kijani na nyeupe, na husomwa qaswida na mashairi yanayo husu mtoto mchanga pia huinuliwa juu mtoto mmoja mchanga kama ishara ya kukumbuka namna Imam Alivyo mnyanyua mwanaye wakati anamuombea maji.

Kitabu cha Arbaabul Maqaatil kinasema: Imam Hussei (a.s) alipo bakia peke yake baada ya kuuawa kwa maswahaba wake na watu wa nyumbani kwake (a.s), alienda katika hema akasema: Nipe mwanangu mchanga, akamchukua na kumlea miguuni, akambusu na kusema: Ole wao watu hawa, atakapo kua babu yako Mtume Muhammad (s.a.w.w) ndiye mgonvi wao.

Bibi Zainabu (a.s) akamuambia kaka yake, ewe Abuu Abdillah, mama wa huyu mtoto maziwa yamekauka kifuani kwake, nenda ukamuombee maji huenda watampa hata kidogo.

Imam (a.s) alipo enda kumuombea maji, maadui wakatofautiana, baadhi yao wakasema apewe na wengine wakasema asipewe huku wengine wanasema; hakuna kumbakiza hata mmoja katika watu wa nyumba hii, Omari bun Saadi aliyekua kamanda mkuu wa jeshi la Yazidi bun Muawiya, akamgeukia Harmala bun Kaahil Asadiy na kumuambia: Ewe Harmala maliza ubishi.

Harmala anasema: Nikaelewa nini anamaanisha kiongozi wangu, nikaingiza mshale katika upinde, nikaanza kuangalia sehemu ya kuchoma, nikaona nichome katika shingo la mtoto, aliye kua amelala mikononi mwa baba yake akiwa kazidiwa na kiu kali, mshale ulipo tua shingoni kwake ulimchinja kabisa, akamkumbatia baba yake akiwa anahangaika kama nyege aliye chinjwa, Hussein akaweka mkono wake chini ya sehemu zilipo kua zinatiririka damu kama bomba kisha akazirisha damu hizo mbinguni huku anasema: Ewe Mola mimi nakushitakia watu hawa, hakika wao wanataka asibakie yeyeto katika kizazi cha Mtume wako.

Imamu Hussei (a.s) akarudi nae kwenye hema, akapokewa na Sukaina huku anasema: huenda baba amempa maji Ablallah na yale yaliyo bakia anatuletea, akasema kumuambia bint yake Sukaina, huyu kaka yako amechinjwa na mshale umemtoboa kuanzia upande wa kwanza hadi wa pili.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: