Picha za juu zinazo onyesha kufurika kwa watu

Maoni katika picha
Picha za juu zinazo onyesha kumiminika kwa vikundi vya waombolezaji (mawakibu) leo siku ya mwezi kumi Muharam (1439h) sawa na (1 Oktoba 2017m) baada ya swala za Dhuhuraini.

Picha hizi zimepigwa na idara ya uzalishaji ofisi ya matangazo ya moja kwa moja chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu.

Ikumbukwe kua wamesha tangaza masafa yanayo rusha shughuli zote za maombolezo bure, katika kipindi cha miezi miwili. wa Muharam na Safar.

Na wakatoa wito kwa vyombo vyote vya habari vya kitaifa na kimataifa vitakavyo penda kurusha matangazo hayo zifuate maelekezo yafuatayo:

SAT: INTELSAT 902@62°E

DL:11193 V

SR:3000

DVBS2

FEC:2/3

HD/MPEG-4


Tunapenda kufahamisha kua; Matembezi ya Tuwarej, ni matembezi ya Husseiniyya ambayo watu huonyesha uwezo wao katika kuomboleza, kwa mara ya kwanza matembezi hayo yalifanywa na watu wa Tuwarej (Wilaya ya Hindiyya katika mkoa wa Karbala, ipo umbali wa kilometa 20), matembezi haya hufanywa kama kuhuisha na kuitikia wito wa Imamu Hussein (a.s), alipo sema: (Je! Yupo wa kuninusuru aje kuninusuru), kwa mara ya kwanza, matembezi haya; yaliandaliwa na taasisi moja na yakawa matembezi yenye watu wengi zaidi duniani, ya yenye muonekano wa aina yake, katika mwaka wa (1303h) sawa na (1885m).

Inasemekana kua; katika siku ya kumi ya mwezi wa Muharam baada ya kumaliza kusoma maqtal katika nyumba ya Sayyid Swaleh Kazwini, lilitoka kundi kubwa la watu huku wanaita (Waa Hussein.. Waa Hussein) tumekuja kumnusuru, wakazunguka katika njia za mji huo, baada ya miaka wakawa wanatoka baada ya swala ya Dhuhurain ambayo wanaiswalia katika Qantwaratu Swalaa, iliyopo umbali wa kilometa tano kutoka katika kaburi la Imamu Hussein (a.s), matembezi hayo huongozwa na watu wa Tuwarej.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: