Mgahawa (mudhifu) wa Abulfadhil Abbasi (a.s) watoa chakula kila siku kwa mazuwaru wa msimu wa Ashura

Maoni katika picha
Miongoni mwa mikakati ya kuwahudumia watu wanaokuja kumzuru Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), katika mwezi wa Muharam ni kugawa chakula kwa mazuwaru, kitengo cha mgahawa wa Atabatu Abbasiyya tukufu, kinagawa maelfu ya sahani za chakula kila siku mara mbili, pamoja na vyakula vidogo vidogo kama vile matunda na vitafunwa (keki, pipi nk).

Sio kwamba wanatoa chakula kwa mazuwaru pekeyao, bali wanatoa pia kwa watumishi na wale wanao jitolea kuhudumia mazuwaru pamoja na wageni wa Ataba, ugawaji wa chakula unafanyika kupitia madirisha yaliyo andaliwa na kitengo hicho kwa ajili ya shughuli hiyo, na kunakua na misululu mikubwa ya kuchukua chakula lakini haileti usumbufu kwa mazuwaru.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu imesha tangaza kukamilika kwa maandalizi yote ya kuwapokea watu wanaokuja kumzuru Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) katika siku ya kumi ya mwezi mtukufu wa Muharam, wamejiandaa kwa kuimarisha usalama na kuboresha huduma, kwa kiasi kwamba watu wanaokuja kufanya ziara wataweza kutekeleza ibada na kufanya ziara kwa amani na utulivu, wanahakikishiwa kupatikana kwa huduma zote muhimu za kibinadamu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: