Atabatu Abbasiyya tukufu yatangaza kufaulu kwa mkakati wake wa uimarishaji wa usalama na uboreshaji wa huduma katika ziara ya Ashura..

Maoni katika picha
Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu umetangaza kufanikiwa kwa mkakati wake wa uimarishaji wa usalama na uboreshaji wa huduma katika kipindi cha ziara ya Ashura, ulio anza kutekelezwa siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Muharam, na ukadumu siku kumi, ukahitimishwa na matembezi ya Tuwarej yanayo shiriki mamilioni ya watu, na wametangaza kuanza rasmi kwa kazi ya kuwachukua mazuwaru katika maeneo ya haram na kuwapeleka kwenye vituo vya usafiri vilivyopo nje kidogo ya mji, kwa ajili ya kuwarahisishia kurudi majumbani kwao.

Haya yalisemwa na makamo katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Muhandisi Bashiri Muhammad Jaasim Rabii, ambaye amesema kua: “Kutokana na juhudi za watumishi wa Atabatu Abbasiyya na wale waliokuja kufanya kazi kwa kujitolea, wamefanikisha mpango wa usalama na uboreshaji wa huduma bila kutokea tatizo lolote la uvunjifu wa amani, lakini haya yoto yamefanikiwa kutokana na baraka za Abuu Abdillahi Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), ziara ya mwaka huu imefanyika kwa ushirikiano mkubwa ulio onyeshwa na watumishi wa Ataba mbili (Husseiniyya na Abbasiyya) tukufu, pamoja na watumishi wa kujitolea bila kuwasahau viongozi wa mawakibu na vikundi vya Husseiniyya walio fuata kwa ukamilifu maelekezo yaliyo tolewa na viongozi wa Ataba mbili tukufu”.

Akaongeza kusema kua: “Atabatu Abbasiyya tukufu, kutokana na juhudi za watumishi wake, imeweza kutoa huduma bora, kila mtumishi alifanya kazi kwa bidii kutokana na kitengo chake na majukumu aliyo pewa, wote wamekua mfano mwema, wakiongozwa na kauli mbiu moja isemayo: (Kumtumikia zaairu ndio fahari yetu na sababu ya kupata radhi za Mwenyezi Mungu mtukufu na radhi za mwenye malalo hii takatifu, Abulfadhil Abbasi (a.s)). Mafanikio haya ni sehemu ya kukamilisha juhudi zilizo tangulia, ratiba ilienda kama ilivyo pangwa bila kikwazo chochote, na tumefikia malengo, ambayo ni kutoa huduma bora na kuhakikisha amani na usalama unatawala na mazuwaru wanarudi salama katika miji yao”.

Akabainisha kua: “Mawasiliano mazuri na Atabatu Husseiniyya tukufu bamoja na idara zote za watumishi wa Ataba mbili tukufu, na ushirikiano imara wa idara za ulinzi na usalama za mkoa wa Karbala ndio sababu kubwa ya mafanikio haya, ambayo tunachukulia kama utangulizi wa maandalizi ya ziara ya Arbainiyya”.

Akamaliza kwa kutoa shukrani kwa vyombo vyote vya ulinzi na usalama katika mkoa wa Karbala na watumishi wote wa Ataba mbili tukufu, pamoja na vikundi vya Husseiniyya vyote bila kuwasahau ofisi za serikali, kwa juhudi kubwa walizo fanya za kuondoa kila aina ya uzito kwa mazuwaru wetu watukufu, akamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu airudishe ziara hii tena tukiwa katika usalama na amani.

Hizi ni sehemu za picha zilizo pigwa na mtandao wa Alkafeel zinazo onyesha matembezi ya Tuwarej na sehemu za huduma zilizo tolewa na Atabatu Abbasiyya tukufu kwa mazuwaru.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: