Usiku wa Muharam kumi na moja, Karbala imejaa huzuni na yawashwa mishumaa

Maoni katika picha
Vumbi la vita limetulia na sauti za panga zimesimama, bado zinasikika sauti za kwato za farasi na sauti ya mvumo wa upepo wa njano inasikika huku familia ya Mtume wa rehema Muhammad (s.a.w.w) ikiwa katika mfadhaiko mkubwa.

Mwenyezi Mungu aitukuze roho yako ewe bibi Zainabu, tunazituma kwako salamu milele kwa muda wote tutakao kua hai usiku na mchana, ulikua katika hali gani ndani ya saa hivi ukiwa katikati ya mayatima, majeruhi na maiti, ewe jabali wa subira, amani iwe nawe milele.

Amani iwe kwako ewe Abuu Abdillah.. na kila aliyejitolea roho yake kwa ajili yako.

Amani iwe kwako ewe Hussein.

Na kwa maswahaba wa Hussein.

Na kwa watoto wa Hussein.

Na kila aliye jitolea nafsi yake kwa ajili ya Hussein (a.s).

Usiku wa mwezi kumi na moja Muharam, Karbala huzizima kwa huzini na huwashwa mishumaa katika njia zake kama ishara ya kuienzi siku hii.

Pamoja na kuhitimisha maombolezo ya Ashura ambayo hudumu siku kumi mfululizo, jioni ya siku ya kumi katika mwezi wa Muharam, vikundi vingi vya maombolezo humiminika kumpa pole bibi Zainabu (a.s), na hukumbuka matatizo aliyo pata katika siku kama ya leo mwaka wa (61h).

Miongoni mwa vikundi hivyo ni kikundi cha makamanda wa Karbala, kikundi kilicho pata muitikio mkubwa sana katika matembezi yao kutoka kwa mazuwaru watukufu, na kuwafanya wahisi huzuni kama walivyo kua watu wa nyumba ya Mtume (a.s) katika siku hii, Ataba mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya) zimewasha taa nyekundu ndani ya kumbi za haram zake kama ishara ya kuienzi siku hii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: