Asubuhi ya leo Juma Tatu ya (11 Muharam 1439h) sawa na (2 Oktoba 2017m) watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) kitengo cha uangalizi wa haram tukufu, wameanza kusafisha milango na ukumbi wa haram.
Kazi hii imeanza baada ya kumaliza siku kumi za maombolezo ya Muharam na ziara ya Ashura pamoja na matembezi ya Tuwarej. Watumishi wa Abulfadhil Abbasi, mapema leo asubuhi wameanza kazi ya usafi kwa kuondoa michanga katika mabusati yaliyopo ndani ya ukumbi wa haram tukufu, pamoja na kutandika upya miswala.
Makamo rais wa kitengo cha uangalizi wa haram Ustadh Haidari Majhuul ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Baada ya kumaliza siku kumi za ziara ya Ashura, pamoja na matembezi ya Tuwarej, tumeanza kusafisha ukumbi mtukufu wa haram kwa kuondoa vumbi na michanga katika milango na ndani ya ukumbi, hali kadhalika tumeondoa kapeti lilotandikwa kwa ajili ya siku kumi za kwanza za mwezi huu wa Muharam na tumetandika miswala (busati) zingine”.
Kazi ya watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) haijaishia hapo tu, kitengo cha utumishi chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu wamefanya kazi ya kusafisha maeneo yote yanayo zunguka haram tukufu pamoja na baadhi ya njia zinazo ingia katika eneo la haram.
Kumbuka kua uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, uliwaweka tayali watumishi wa vitengo vyote kwa ajili ya kuhuisha ziara ya Ashura, na kutoa huduma bora zaidi kwa watu wanaokuja kumzuru Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).