Ujumbe kwa mateka wa Twafu

Maoni katika picha
Amani iwe kwao mateka, amani iwe kwao watu wa nyumba ya utume na mabibi wa wanawake, familia ya bwana wa mawasii, amani iwe kwake Aqila mtukufu Zainabu binti Amirulmu-uminina na Sukaina binti wa Imamu Hussein, na Ummu Kulthum binti wa Amirulmu-uminina na Fatuma binti Hussein na Fatuma binti Imamu Hassan mke wa Imamu Ali Sajjaad, na Rubaab na mke wa Aqiil bun Abutwalib, pamoja na walio kua nao katika wanawake, na mayatima, pamoja na familia za mayatima wa maswahaba wake.

Ujumbe gani mliotoa kwa walimwengu hadi mkabadilisha kuuawa kwa Hussein kua mapinduzi (thaura), mlipo pitishwa na maadui katika miji mkiwa ni mateka? Roho mbaya, unyama na ujinga ulioje wa watu walio kutekeni, hawakujali haiba na heshima ya Mtume na watu wa nyumbani kwake (a.s), wakakuzungusheni mji mmoja hadi mwingine, watu hao walio kutekeni walishindwa na kudhalilika, historia imewatupa jalalani, baada ya kuthubutu kujaribu kuvunja harakati ya Imamu Hussein (a.s) na kukudhalilisheni, na nyie mkawaonyesha subira ya hali ya juu kabisa, mliwafanyia ubaya gani hadi wao wawateke na kuwatesa? lakini mbingu ilikufunikeni ikawa ni stara yenu juu ya mavazi yenu na aridhi ikajikunja chini ya nyayo zenu kupunguza urefu wa safari ya mateka.

Hadi leo bado harakati ya Imamu Hussein (a.s) inaendelea, na maadui wa ubinadamu wanajaribu kupambana na wafuasi wa Ahlulbait muda wote na kila sehemu, lakini walishindwa na wanaendelea kushindwa, nyumba ya Mola anaihami na umma lazima uwe na viongozi wema, hawa hapa wanusuruji wenu wanaofuata nyayo zenu, na kuiga subira yenu, wanaonyesha igizo la mateka na kumpa pole bibi Amina, Khadija, Zaharaa, Zainabu na Ummul-Banina, kwa yaliyo tokea katika siku hizo chungu, amani iwe kwenu enyi mlio onyesha subira kubwa katika mtihani mliopewa na Mola wa walimwengu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: