Zaidi ya watu elfu kumi na moja wamefanyiwa ziara ya Ashura kwa niyaba..

Maoni katika picha
Ustadh Haidari Mamitha mhariri mkuu wa mtandao wa Alkafeel (mtandao ramsi wa Atabatu Abbasiyya) ametangaza kua; idadi ya watu walio jisajili katika ukurasa wa ziara kwa niaba na wakafaniwa ziara na kusomewa dua katika siku ya Ashura imefika (11,100), walisajiliwa katika kumi la kwanza la mwezi mtukufu wa Muharam, kupitia mtandao wa kimataifa wa Alkafeel katika lugha zake zote: (Kiarabu, Kiengereza, Kiurdu, Kituruki, Kifaransa, Kiswahili na Kijerumani).

Akaongeza kusema kua: “Asilimia kubwa ya watu walio jisajili wametoka katika nchi zifuatazo: (Iraq, Iran, Lebanon, Pakistan, Urusi, Marekani, Uingereza, India, Saudia, Swiden, Kanada, Kuwait, Malesia, Australia, Aljeria, Baharain, Misri, Ujerumani, Islandi, Namsa, Yunani, Holandi, Tunisia, Denmak, Norwey, Qatar, Ubelgiji, Komoro, Afghanistan, Oman, Ekwado, Brazili, Ajentina, Uswisi, Naijeria, Gana, Yemen, Indonesia, Italia, Hispania, Ufaransa, Uturuki, Adharbaijan, Finland, China, Ailend, Hong Kong, Japani, Falme za kiarabu na Sudani)”.

Akabainisha kua: “Hakika ziara ilihusisha utekelezaji wa ibada zinazo fungamana na ziara, ikiwa ni pamoja na swala ya rakaa mbili na kusoma dua, akasisitiza kua; ukurasa wa ziara kwa niaba uko wazi kwa kila anayetaka kujisajili kwa ajili ya kufanyiwa ziara, pia anaweza kutumia lugha yeyote miongoni mwa lugha zilizopo katika mtandao wetu, na anaweza kuhakiki jina lake katika ukurasa huo huo”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: