Mawakibu za watu wa Karbala za kutoa huduma ni alama ya ukweli kuhusu ukarimu wa Imamu Hussein (a.s)..

Maoni katika picha
Watu wa Karbala tangu zamani wamejenga mazoea vizazi na vizazi ya kufanya maombolezo na kutoa huduma katika siku kumi za mwanzo katika mwezi mtukufu wa Muharam, jambo hili halizuwii ushiriki wa watu wengine, lakini wao ndio watu wa mwanzo katika swala hili, utawaona kabla ya kuingia mwezi mtukufu wa Muharam wanafanya maandalizi ya kutoa huduma kwa watu watakao kuja kufanya ziara kwa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), Maukibu za watu wa Karbala sawa na Mawakibu zingine za Husseiniyya, hufanya maombolezo na kutoa huduma, kuanzia siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Muharam, utawaona wanashindana katika kufanya kazi watoto kwa wazee, wasichana kwa wavulana, wanawahudumia watu wanaokuja kufanya ziara (mazuwaru) kwa kuwapa chakula, vinywaji, sehemu za kulala nk. Huduma hizo huendelea hadi Muharam kumi, na hubakia hadi siku ya kumbukumbu ya kuzikwa kwa Imamu Hussein (a.s) mwezi kumi na tatu Muharam.

Hufanya kila wawezalo katika kutoa huduma kwa watu wanaokuja kufanya ziara, utawaona wamevalia nguo nyeusi, wako bize na kuandaa chakula na vitu vingine miongoni mwa mahitaji muhimu ya mwanadamu, kumbuka huduma zote wanatoa bure, wanatarajia thawabu kwa Mwenyezi Mungu na kuwaridhisha watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w).

Hali ya mazingira inasema, kila tunacho miliki tumekipata kutokana na utukufu wa Abuu Abdillahi Hussein (a.s), na kila tunachotoa kwa watu wanaokuja kufanya ziara ni kidogo ukilinganisha na aliyoufanyia uislamu na ubinadamu, kumhudumia Imamu Hussein (a.s) ni utukufu kwetu duniani na akhera.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: