Mji mtukufu wa Karbala leo (13 Muharam 1439h) sawa na (04 Oktoba 2017m), umeshuhudia kumiminika kwa Mawakibu (makundi) ya watu wa kabila la Bani Asadi pamoja na makabila mengine ya wairaq, waliokuja kuhuisha kumbukumbu ya kuzikwa kwa mwili mtakatifu wa Bwana wa Mashahidi na watu wa nyumbani kwake (a.s), pamoja na maswahaba zake walio uawa katika vita ya Twafu mwaka wa 61 hijiriyya.
Riwaya zinasema kua; siku ya tatu baada ya kuuawa kishahidi kwa Imamu Hussein na watu wa nyumbani kwake (a.s), kundi la wanawake wa Bani Asadi walifika katika eneo hilo, wakakuta miili ya watu ikiwa juu ya aridhi bila kuzikwa na haina vichwa, hakika mazingira yalikua yanatisha sana, haujawahi tokeo unyama wa aina hii katika historia ya mwanadamu, ndipo Bani Asadi wakatoka na vifaa vya kuzikia, walipo fika walitahayari; wanaona mbele yao maiti zimelala zikiwa hazina vichwa, hawajui huyu nani na yule nani!? Wakiwa katika hali hiyo; akatokea Imamu Zainul-Abidina, akajitambulisha kwao na akawaomba wamsaidie kuzika miili hiyo mitakatifu, hivi ndio inavyo ripoti historia namna Bani Asadi walivyo shiriki kuwazika mashahidi hao watukufu.