Wanawake wa Iraq wanatoa rambirambi zao kwa Hauraa na kufanya maombolezo ya mazishi..

Maoni katika picha
Baada ya kufuata mwenendo wake (a.s) aliye jitolea watoto wanne kwa ajili ya kumuhami na kumlinda Imamu Hussein (a.s), aliye jutoa muhanga baada ya kuona uislamu upo katika hatari, na wao wametoa watoto wao baada ya kusikia aridhi iliyo kumbolewa na Imamu Hussein (a.s) inaomba msaada.

Leo katika maombolezo ya kumbukumbu ya kuzikwa kwa Imamu Hussein na watu wa nyumbani kwake (a.s), kundi kubwa la wanawake wameenda kumpa pole bibi Zainabu (a.s), wakiwa wamebeba picha za mashahidi walio mwaga damu zao kwa ajili ya kulinda aridhi ya nchi hii na maeneo yake matakatifu.

Picha nyingi walizo beba ni za mashahidi wa Hashdi Sha’abi, hususan watu wa hauza tukufu ya Najafu, walio poteza maisha yao kwa ajili ya kutetea uhuru na haki, ambao ulikua ndio mwenendo wa Imamu Hussein (a.s) katika harakati yake, jina la Karbala linafungamana na maana ya shahada, na ushindi wa damu dhidi ya upanga, na haki dhidi ya batili, huku wanakumbuka mazingira ya ushujaa, jihadi na kujitolea, na hawakuja peke yao; bali, wamekuja na waume zao pamoja na watoto wao kumpa pole bibi Zainabu, Rubaab na Sukaina (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: