Mwaka wa nne mfululizo: Maukibu ya taa za mbinguni yafanya kumbukumbu ya siku ya tatu ya kuuawa kwa Imamu Hussein (a.s)..

Maoni katika picha
Kumbukumbu ya yaliyojiri katika siku kama ya leo mwaka (61) hijiriyya, kama kawaida mwaka wa nne mfululizo, baada ya swala za Magharibi na Isha, Maukibu ya taa inayo undwa na watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) ilianza matembezi, wakiwa na baadhi ya watoto waliovaa nguo nyeupe na kubeba mabango yaliyo andikwa majina ya mashahidi wa Twafu, kuanzia jina la Imamu Hussein na watu wa nyumbani kwake (a.s) pamoja na maswahaba zake watukufu.

Matembezi yalianzia katika mlango wa Kibla wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), wakapita katika ukumbi mtukufu wa haram, wakiwa wametanguliwa na wabeba bendera na misahafu, wakaelekea katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, wakaenda hadi katika kaburi la Imamu Hussein (a.s), walipo fika huko wakafanya majlis ya maombolezo na wakatuma rambirambi zao kwa Imamu wa zama Mahdi (a.f) kutokana na tukio hili chungu.

Kumbuka kua mji mtukufu wa Karbala leo, baada ya swala ya Adhuhuri na Alasiri, ulishuhudia maombolezo ya kumbukumbu ya kuzikwa Imamu Hussein (a.s), yaliyo ongozwa na kabila la Bani Asadi wakishirikiana na makabila mendine ya Karbala na miji inayo zunguka mji huu mtakatifu, ikiwa ni kumbukumbu ya siku ya tatu baada ya kuuawa kwa Imamu Hussein na watu wa nyumbani kwake (a.s) pamoja na maswahaba wake watukufu, na ndio siku iliyo zikwa miili yao mitakatifu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: