Kwa lengo la kuandaa kizazi bora, Atabatu Abbasiyya tukufu yafungua chuo kikuu huria cha wanawake..

Maoni katika picha
Kwa ajili ya kuandaa na kutengeneza kizazi cha wasomo bora wa kike, watakao weza kufikisha sauti ya harakati ya Imamu Hussein (a.s) kila sehemu ya dunia, na wahadhiri bora wa kidini, Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia kitengo cha habari na utamaduni imefungua chuo cha wanawake cha masomo ya mtandaoni (Chuo huriya) kiitwacho: Ummul-Banina (a.s) (Jaamiatu Ummul-Banina (a.s) Al-Iktroniyya li-I’daad mubalighaat).

Ufunguzi wa chuo huki umetokana na mafanikio makubwa yaliyo patikana katika Maahadi huriya ya turathi za mitume (Maahadi turathul-anmbiyaa (a.s) lidirasaat hauzawiyya al-iktroniyya), na kutokana na ongezeko kubwa la watu wanao jiunga na Maahadi hiyo kutoka kila sehemu ya dunia, ukizingatia kua kizuizi kikubwa cha wao kupata elimu kilikua ni umbali wa masafa kutoka sehemu wanazo ishi na kuja katika mji mtukufu wa Najafu kisima cha elimu na maarifa, kizuizi hicho kimeondolewa baada ya kuanzishwa masomo ya mtandaoni (masafa), uzoefu huo umehamishiwa katika kuanzisha chuo maalumu cha kuandaa wataalamu wakike watakao saidia kusambaza malengo ya harakati ya Imamu Hussein (a.s) katika mihadhara yao itakayo jaa weledi na maarifa.

Muda wa masomo katika chuo hiki ni myaka minne, miaka mitatu ya kwanza itakua ya kusoma kwa nadharia na mwaka wa nne watasoma kwa vitendo, wataenda kutoa mihadhara sehemu mbalimbali ndani na nje ya Iraq, na watasomeshwa kwa kufuata selibasi iliyo andaliwa na walimu wa hauza ya Najafu.

Kila anayependa kujiunga na chuo hiki anaweza kujaza fomu iliyopo katika mtandao wetu ufuatao: http://turath-alanbiaa.org/um-albanien/login/signup.php

Muombaji natakiwa awe na sifa zifuatazo:

  • 1- Awe na shahada ya sekondari (I’daadiyya) au shahada yeyeto inayo lingana na hiyo.
  • 2- Asiwe chini ya myaka (20) na sio zaidi ya myaka (45).
  • 3- Awe na barua ya utambulisho (tazkiya) kutoka kwa wakili wa Marjaa au mtu maarufu anaye julikana katika ofisi ya chuo hiki.
  • 4- Afaulu mtihaji wa majaribio kwa kupata alama zisizo pungua (60%) atakao pewa na kamati ya mapokezi katika Atabatu Abbasiyya.

Mwanzo wa mwaka wa masomo utakua 4 Shawwal 1439h, na ndio mwanzo wa mwaka wa masomo katika kila mwaka, muda rasmi wa masomo ni siku tano kwa wiki, na kila siku inavipindi vitatu, kila kipindi kinachukua kati ya dakika (30 hadi 45).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: