Baada ya safari iliyo dumu siku 14 kwa baskeli, Zaairu kutoka Adharbaijan awasili katika Ataba za Karbala tukufu na asisitiza kua kumpenda Hussein kumemfupishia masafa..

Maoni katika picha
Baada ya safari iliyo dumu siku 14 kwa baskeli, asubuhi ya Ijumaa ya leo (15 Muharam 1439h) sawa na (06/10/2017m), Zaairu kutoka Adharbaijan bwana Zaihuun Husseiniy amewasili katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), akiwa katika harakati ya kukamilisha ratiba yake ya kiibada kwa kwenda kuzuru malalo ya Imamu Hussein (a.s) na maimamu wengine waliozikwa hapa Iraq.

Husseiniy ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Nimekuja Iraq nikiwa nimebeba salamu na rambirambi kutoka kwa wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) wa Adharbaijan kufuatia kuuawa kishahidi kwa Abuu Abdillahi Hussein na watu wa nyumbani kwake (a.s) pamoja na maswahaba wake, safari yangu imedumu siku 14, nimepita katika jamhuri ya Iran kisha nikaingia katika nchi ya manabii na mawasii, nchi ya Iraq, kwa kupitia Mkoa wa Waasit, na sasa nakamilisha safari yangu kwa kuwasili katika mji wa Shahada Karbala na nimenawirisha macho yangu kwa kuangalia Kubba hizi takatifu”.

Akaongeza kusema kua: “Katika safari hii natarajia kuzuru malalo ya Imamu Ali (a.s) na malalo ya matakatifu ya Jawadaini na Askariyaini (a.s), na nitakuja tena katika ziara ya Arbainiyya”.

Husseiniy akasisitiza kua: “Hakika mapenzi yangu kwa Imamu Hussein (a.s), yamefanya masafa haya marefu kua mafupi, wala sijapata ugumu wowote katika safari yangu, pia nimeona tofauti na matarajio, kutokana na tunayo sikia katika habari kuhusu Iraq na uwepo wa kundi la kigaidi la Daesh, marafiki zangu wengi walinitahadharisha kuhusu safari hii kutokana na kukosekana kwa amani hapa Iraq, sikutarajia kuona niliyo yaona katika safari yangu hapa Iraq, nimepokelewa vizuri sana, nimepewa kila aina ya msaada ili kunirahisishia rafari”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: