Baada ya kukomboa mji wa Riyaadh, kikosi cha Abbasi chaenda kaskazini ya mji wa Huweijah kuungana na vikosi vingine..

Maoni katika picha
Kikosi cha Abbasi (a.s) brugedi ya (26) kimetangaza kukamilisha jukumu walilo pewa la kukomboa mji wa Riyaadh uliopo kusini mashariki ya mji wa Huweijah kilometa (18) kutoka makoa makuu ya wilaya, na wakasafisha mabaki yote ya Daesh kisha wameelekea kaskazini ya mji wa Huweijah kwa ajili ya kuungana na vikosi vingine huko na kuendelea na mapambano. Eneo lililo kombolewa linaukubwa wa zaidi ya kilometa (120), linajumuisha vijiji vyenye umuhimu mkubwa kijeshi, hakika kikosi bado kinaendelea kusonga mbele.

Kumbuka kua kikosi cha Abbasi (a.s) kwa kushirikiana na jeshi la anga wamefanikiwa kukomboa mji wa Riyaadh uliopo kusini mashariki ya wilaya ya Huweijah kutoka mikononi mwa Daesh, katika opreshen ya (Tunakuja ewe Huweijah) awamu ya pili.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: