Maahadi ya Qur’an tukufu tawi la Najafu yatengeneza program inayo saidia wanafunzi kuhifadhi Qur’an tukufu.

Maoni katika picha
Kwa ajili ya kukuza uwezo wa kiakili na kuwasaidia wanafunzi katika kuhifadhi Qur’an tukufu, Maahadi ya Qur’an katika mkoa wa Najafu chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu imetengeneza program ya kiakili inayo saidia kukuza uwezo wa kuhifadhi Qur’an kwa urahisi.

Mkuu wa tawi la Maahadi Sayyid Mahandi Almayali amesema kua: “Kuna njia nyingi zinazo saidia kuhifadhi Qur’an tukufu, kutokana na umuhimu wa swala hili, tumetengeneza program ya mchezo unao ongeza uwezo wa kuhifadhi kwa mwanafunzi chini ya usimamizi wa mwalimu, mtaalamu wa program hiyo. Mwanafunzi atafanya mchezo huo baada ya kusikilizwa hifdhu yake ya kila siku na mwalimu”.

Akaongeza kusema kua: “Baada ya kufanya utafiti wa kina kuhusu mchezo huu umeonyesha kua unasaidia kwa kiasi kikubwa mambo yafuatayo:

  • 1- Unakuza uwezo wa kumbukumbu.
  • 2- Unakomaza uwezo wa akili.
  • 3- Unachangamsha kumbukumbu kwa haraka (ya muda mfupi).
  • 4- Unaongeza ari ya kushindana na kuchangamsha akili na mazingatio.
  • 5- Unasaidia kujifunza hatua sahihi za kufikia katika lengo.
  • 6- Unamfundisha mwanafunzi namna ya kufanya maamuzi sahihi yatakayo msaidia kufikia lengo.
  • 7- Unaongeza uwezo wa mwanafunzi katika kuhifadhi Qur’an tukufu.

Akamalizia kwa kusema kua: baada ya majaribio yaliyo onyesha mafanikio makubwa, sasa hivi program hii imehusisha wanafunzi wote, na imeleta mafanikio makubwa zaidi. Tupo tayali kushirikiana na taasisi yeyote inayo jishughulisha na mambo ya Qur’an na kuwasaidia katika hili”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: