Kikosi cha Abbasi (a.s): Tumefikia malengo yote katika vita ya kukomboa mji wa Huweijah ndani ya muda uliopangwa..

Maoni katika picha
Viongozi wa kikosi cha Abbasi (a.s) wamesema kua: Tumekamilisha majukumu yote tuliyo pangiwa na wakuu wa jeshi katika vita ya kukomboa mji wa Huweijah ndani ya muda ulio pangwa, ambao ulikua ngome ya mwisho ya Daesh kaskazini ya Iraq, mafanikio haya yanachangia pakubwa katika kumaliza upatikanaji wa Daesh nchini Iraq.

Wapiganaji wameonyesha ushujaa na ujasiri wa hali ya juu kabisa na wamewapa hasara kubwa ya mali na nafsi magaidi ya Daesh.

Majemedari hawa kutokana na uzowefu wao katika vita na mbinu za kivita, wamefanikiwa kukomboa zaidi ya kilometa 750 katika maeneo ambayo magaidi wa Daesh walikua wanayatumia kama sehemu zao tegemezi katika kushambulia, pia wamekomboa zaidi ya vijiji 60 na wameua makumi ya magaidi na kuripua mapomu mengi yaliyo kua yametegwa na magaidi hao.

Opreshen hii imefanyika kwa kusaidiana na jeshi la anga pamoja na kikosi cha 34 cha jeshi la Iraq.

Wakuu wa kikosi cha Abbasi (a.s) wamesema kua wako tayali kutekeleza akizo lolote litakalo elekezwa kwao wakati wowote.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: