Daru Rasuul A’dham yatangaza mada za kongamano lake la kielimu na kimataifa awamu ya kwanza na yaomba ushiriki wa watafiti..

Maoni katika picha
Daru Rasuul A’dham (s.a.w.w) chini ya kituo cha Ameed Duwaliy Lilbuhuthi Wadirasaat katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imetangaza mada za kongamano lake la kwanza la kielimu na kimataifa, litakalo fanyika chini ya kauli mbiu isemayo: (Mtume kutoka kwa Mwenyezi Mungu anaye wasomea kurasa zilizo takasika), na chini ya anuani: (Sira ya mtume ni sheria ya Mungu inayo muongoza mwanadamu) litakalo fanyika (3-4 Dhulhijjah 1439h) sawa na (16-17 Agosti 2018m).

Kongamano hili la kimataifa; ni la kwanza kuzungumzia sira ya Mtume, linafanyika sanjari na juhudi za Atabatu Abbasiyya tukufu za kutilia umuhimu wa elimu na utafiti katika sekta mbalimbali, pamoja na kufanya makongamano ya kielimu yanayo endana na mazingira ya sasa, kongamano hili linalenga kuamsha fikra za watafiti na kuzifanya zizingatie sera ya Mtume (s.a.w.w), na kuchukua yanayo paswa kuchukuliwa katika sira yake tukufu, ukizingatia kua ndio muongozo unaofaa kufatwa na jamii na una athari katika kuelekeza mambo ya waislamu wa zama zetu, maelekezo yanayo oana na mafundisho ya Qur’an tukufu.

Daru inatoa wito kwa watafiti wote na wasomi washiriki katika kongamano hili, litakalo kua na mada zifuatazo:

 • 1- Masomo ya Qur’an na Aqida:
 • - Sira ya Mtume katika uongofu wa Qur’an tukufu.
 • - Sira ya Mtume katika mtazamo wa Ahlulbait (a.s).
 • - Riwaya za sira ya Mtume katika mtazamo wa waislamu kifikra na ki-aqida.
 • - Mtume Mtukufu (s.a.w.w) katika dini zingine.
 • 2- Masomo ya kihistoria:
 • - Sira ya Mtume katika uandishi wa historia.
 • - Sira ya Mtume katika masomo ya wasiokua waislamu.
 • - Utukufu wa Mtume katika vitabu vya watu wenye mtazamo wa fitina.
 • - Yaliyo hifadhiwa (andikwa) katika sira ya mtume.
 • 3- Masomo ya lugha la adabu:
 • - Sira ya mtume katika vitabu vya lugha na adabu.
 • - Picha ya Mtume (s.a.w.w) katika vitabu tofauti vya lugha.
 • - Hadithi za Mtume (s.a.w.w) katika fani za lugha na adabu.
 • 4- Masomo ya malezi na kijamii:
 • - Misingi ya malezi na tabia njema katika sira ya Mtume.
 • - Sira ya Mtume katika selibasi za masomo.
 • - Jambo la mwisho katika sira ya Mtume.
 • - Masomo ya siasa na uchumi.

Masharti ya kushiriki ni:

 • 1- Mtafiti azingatie kanuni za kielimu, na utafiti ukidhi vigezo vya kielimu.
 • 2- Aandike utafiti wake kwa kiarabu au kiingereza.
 • 3- Utafiti wake uwe haujawahi kuandikwa na mtu mwingine (asikopi na kupesti).
 • 4- Aandike muhtasari wa utafiti wake katika ukurasa mmoja kwa kiarabu na kiingereza, na ahifadhi utafiti wake katika (CD), mwanzo wa kupokelewa tafiti hizo ni 15/05/2018m na mwisho ni 15/05/2018m.
 • 5- Utafiti uandikwe kwa kutumia program ya (Word) hati ya (Simplified Arabic) ukubwa wa hati uwe saizi 14 na zisizidi kurasa 25 pamoja na wasifu (cv) wa mtafiti.
 • 6- Itaundwa kamati ya wataalamu watakao pitia tafiti hizo na kuzichuja, fahamu kua tafiti zitakazo chaguliwa kushiriki katika kongamano hazitazidi 20.
 • 7- Tafiti zitakazo pasishwa kushiriki zitafanyiwa rudufu (zitachapishwa) kwa idadi maalum kwa ajili ya washiriki wa kongamano.
 • 8- Atabatu Abbasiyya tukufu itagharamia makazi ya watafiti na wageni watakao kuja kutoka nje ya Iraq.

Tunasubiri tafiti zetu tukufu, mnaweza kuzituma kwa kutumia anuani ifuatayo:

daralrasul@alameedcenter.iq

Kwa maelezo zaidi piga simu zifuatazo:

07602355555 – 07602323337 – 07719487257.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: