Kikosi cha Abbasi (a.s) cha shindikiza vijana wanne katika pepo ya milele walio pata shahada katika vita ya kukomboa mji wa Huweijah..

Maoni katika picha
Kikosi cha Abbasi (a.s) kimeshindikiza vijana wake wanne kwenda katika pepo ya milele ambao ni, (Shahidi Haji Abbasi Hussein Abidaan Tamimi, Shahidi Muhammad Shaatwiy Khaikaaniy, Shahidi Haidari Taufiq Tamimi na Shahidi Murtadha Jabaru Shaibaani) walio pata shahada katika vita ya kukomboa mji wa Huweijah.

Swala ya jeneza zao iliongozwa na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi ndani ya ukumbi wa haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu ulitoa tangazo la msiba hao ndani ya haram tukufu, ifuatayo ni nakala ya tangazo:

“Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu, Hakika sote ni wa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea, Hakuna hila wala nguvu ispokua ni za Mwenyezi Mungu mkuu, (Wala kabisa usiwadhanie walio uliwa katika njia ya Mwenyezi Mungu kuwa ni maiti, Bali hao ni hai, wanaruzukiwa kwa mola wao mlezi.) Atabatu Abbasiyya tukufu kwa huzuni na masikitiko makubwa, tunatangaza kuuawa kishahidi kwa wapiganaji wetu wa kikosi cha Abbasi (a.s), tunamuomba Mwenyezi Mungu awaweke katika pepo ya milele na awape rehema zake, hakika yeye ni mwingi wa kusamehe na mwingi wa rehema, hakuna hila wala nguvu ispokua ni za Mwenyezi Mungu mkuu”.

Kumbuka kua kikosi cha Abbasi (a.s) kimepata utukufu wa kushiriki katika vita ya kukomboa mji wa Huweijah, na kimepata ushindi mkubwa katika vita hiyo, kimewapa hasara kubwa ya mali na nafsi magaidi ya Daesh.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: