Kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kinajitahidi kuhakikisha kinasambaza vituo vyake vya elimu katika eneo lote la mkoa mtukufu wa Karbala, hususan maeneo yenye wakazi wengi na yenye haja ya vituo vya malezi na elimu, kutokana na juhudi hiyo; shule ya msingi Nurul-Ameed imeingia katika orodha ya vituo vyake katika mwaka huu wa masomo.
Ufunguzi wa shule hii unatokana na kukubalika kwa vituo vya elimu vilivyo chini ya Ameed, kufuatia kufanya vizuri katika ngazi ya mkoa, na kua shule zinazo fanya vizuri katika ngazi ya msingi na sekondari (upili) kitaifa, pamoja na huduma bora walizo nazo, kimalezi, kielimu, mazingira ya masomo, zinafundisha pia hadi kwa njia ya mitandao na inazingatia sana kutozidisha idadi ya wanafunzi katika darasa.
Shule hii ipo kaskazini ya makao makuu ya mkoa wa Karbala, upande wa barabara ya kwenda Bagdad karibu na mtaa wa Abbasi (a.s), ili itoe huduma katika kijiji cha Atwishi na Jariyya, shule imejengwa kisasa kabisa, inamazingira mazuru ya kusomea na vifaa bora vya kujifunzia, pia wamefungua program za kufundisha kwa kutumia mitandao ya Intanet na wana walimu bora.
Kumbuka kua shule za Ameed zipo chini ya kitengo cha malezi na elimu ya juu cha Atabaatu Abbasiyya tukufu, kitengo hiki kinamiliki shule kumi na tatu ambazo ni: Shule ya msingi ya wavulana ya Ameed, Shule ya msingi wa wasichana Ameed, Shule ya msingi ya wavulana Saaqi, Shule ya msingi ya wasichana Alqamaru, Shule ya msingi ya wavulana Sayyidul-Maau, Shule ya Abuutwalib inayo toa mafunzo ya msingi kwa wanaume, Sekondari ya wavulana ya Sayyidul-Maau, Sekondari ya wasichana ya Ameed, Shule ya msingi ya wavulana Nurul-Ameed, Shule ya wavulana Nurul-Abbasi, Shule ya wasichana Nurul-Abbasi na sekondari ya wasichana Nurul-Abbasi. Pia kina club tatu za michezo ya watoto, ambazo ni: Club ya michezo ya Ameed, Club ya michezo ya Saaqi na Club ya michezo ya Nurul-Abbasi.