Maahadi ya Qur’an tukufu yafanya nadwa kuhusu mwenendo wa haki, kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi kitakasifu.

Maoni katika picha
Bado Maahadi ya Qur’an tukufu iliyo chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu inaendelea kufanya nadwa na harakati za Qur’an, miongoni mwa harakati hizo ni nadwa iliyo fanyika hivi karibuni katika tawi lake la Bagdad, katika uwenyeji wa husseiniyya ya Ya’qub katika eneo la Baaji, iliyo kua na anuani isemayo: (Mwenendo wa haki, kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi kitakasifu), na kuhudhuriwa na wadau muhimu wa Qur’an, wasomi na watafiti wa mambo ya Qur’an.

Mtoa mada alikua ni Shekh Dhiyaau-Dini Aali Maajid Zubaidiy mkuu wa kituo cha maarifa ya Qur’an, kuifasiri na kuichapisha chini ya Maahadi ya Qur’an tukufu katika Atabatu Abbasiyya, alifafanua mwenendo wa haki na umuhimu wake kwa watu wanaowajibikiwa na sheria, na akawajulisha kua Maahadi ya Qur’an tukufu imetoa kitabu hivi karibuni chenye jina hilo, ambacho kimeandikwa baada ya kupata maombi kutoka kwa waumini wengi ya kuandika kitabu cha aina hiyo ili wawe na ushahidi utakao wasaidia katika kubaini njia ya haki na kuacha njia ya batili.

Nadwa ilikua na michango mingi pamoja na maswali, mtoa mada alijibu maswali na kufafanua mambo yaliyo hitaji ufafanuzi.

Washiriki wa nadwa walitoa shukrani nyingi kwa Atabatu Abbasiyya tukufu na kwa Maahadi ya Qur’an kwa kufanya nadwa hii muhimu ambayo imeamsha hisia zao kuhusu Qur’an. Na wakaomba ziendelee kufanywa nadwa kama hii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: