Chuo cha Ameed chatangaza kiwango cha max zinazo kubaliwa katika michepuo yake..

Maoni katika picha
Chuo cha Ameed chini ya kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimetangaza kiwango cha max za mwisho kupokelewa katika michepuo yake mitatu (Uganga – Uganga wa meno na Uuguzi) kutokana na maelekezo ya wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu kama ifuatavyo:-

  • 1- Uganga………………….….95
  • 2- Uganga wa meno……….85
  • 3- Uuguzi………………..…….70

Mwanafunzi atapokelewa kulingana na viwango vya max vilivyo tajwa, wanapewa kipawa mbele wenye max za juu zaidi kisha za chini yake kisha za chini, masharti na muda wa kutuma maombi utatangazwa baada ya kupewa mamlaka hayo na wizara ya elimu ya juu na utafiti wa kielimu, kitafunguliwa kituo cha kupokea maombi ndani ya ukumbi wa chuo, na chuo kitakua na haki ya kupokea maombi kwa njia ya mtandao kupitia anuani tutakayo pewa na wizara, itaitwa dirisha la maombi, dirisha hili ndio litakalo husika na kupokea maombi kama tulivyo taja.

Kumbuka kua chuo kikuu cha Ameed ni taasisi ya kielimu iliyo chini ya kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, na kimesha pewa kibali na wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu, kinajitahidi kua jabali la elimu na kuchuana na vyuo vikuu vingine vikubwa, kinafuata vigezo vya kielimu vitakavyo kifanya kua chuo bora.

Chuo kipo katika mkoa mtukufu wa Karbala – mwanzo wa barabara ya Karbala – Najafu karibu na nguzo, kimesajiliwa kwa namba (1238), kwa maelezo zaidi piga simu namba (07602403019) au wasiliana nasi kwa email (info@alameed.iq) kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa kumi jioni.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: