Uongozi wa kikosi cha Abbasi (a.s) umetangaza kukamilika kwa jukumu lake katika opreshen ya tunakuja ewe Huweijah, tangazo hilo limetolewa kwenye kikao na waandishi wa habari kilicho fanyika leo Juma tatu (18 Muharam 1439h) sawa na (9 Oktoba 2017m) katika mji wa Bashiri moja ya viunga vya Karkuki, katika kikao hicho mkuu wa kikosi Shekh Maitham Zaidiy amebainisha mambo mengi, kwa ufupi kaelezea mafanikio yaliyo patikana katika vita hii, miongoni mwa aliyo sema ni:
- - Tulishiriki katika awamu ya pili ya vita ya kukomboa wilaya ya Huweijah pamoja na vitongoji vyake.
- - Lengo letu lilikua ni kukomboa kitongoji cha Riyaadh na kwenda hadi katika sehemu inayo lindwa na Bashimerga.
- - Tulipambana kwa kushirikiana na jeshi la Iraq kikosi cha 34.
- - Tulifanikisha kukomboa eneo la kilometa (41) wakati eneo lote jumla linalo takiwa kukombolewa ni kilometa (246).
- - Tumekomboa vijiji (61), tumeua na kuteka magaidi wengi wa Daesh, pia tulitoa ulinzi imara kwa raia wema.
- - Tumeripua mabomu mengi yaliyo tegwa na adui na tumeteka maghala mengi ya siraha zao.
- - Vita ilienda vizuri na tumewapa hasara kubwa ya roho na mali magaidi ya Daesh.
- - Tuligundua makaburi ya miili ya wapiganaji wetu katika maeneo hayo.
- - Hadi sasa tumemaliza jukumu tulilo pewa katika mji wa Karkuk.
- - Tunasubiri maelekezo mengine kutoka kwa wakuu wa jeshi.
- - Tupo tayari kushiriki katika opreshen yeyote ya kijeshi tutakayo ambiwa kwa sababu tupo katika vita dhidi ya magaidi wa Daesh.