Katika siku kama ya leo mwaka wa 61 hijiriyya mateka kutoka katika msafara wa Imamu Hussein (a.s) walianza safari ya kutoka Kufa na kwenda Sham..

Maoni katika picha
Msiba na misukosuko haikuishia mwezi kumi Muharam mwaka 61 hijiriyya, iliendelea hadi ilipo kuja dhihiri hatua mpya ya mapinduzi na kufanyiwa kazi mtazamo wa Ashura ulio anzishwa na kuimarishwa kwa damu takasifu ya Imamu Hussein (a.s).

Katika siku kama ya leo mwezi kumi na tisa Muharam, msafara wa mateka uliondoka Kufa na kuelekea Sham, baada ya bun Ziyadi kuwaweka jela yenye mazingira magumu na kuzuia watu wasiende kuwatembelea au kuwaona, kutokana na hofu aliyo kua nayo, watu wasije kumbadilikia, kwani tayali watu walikua wanamlaumu na kumshutumu kwa unyama alio fanya, na ukweli ulikua umeanza kujulikana kuhusu ugaidi wa utawala wa bini Umayya.

Walikaa jela siku saba wakiwa hawajui hatima yao, huku bun Ziyadi akiwa ametuma ujumbe kwa Yazidi akimuuliza cha kuwafanya mateka hao, likaja jibu kua mateka wapelekwe Sham pamoja na kichwa cha Imamu Hussein (a.s) na watu wote walio uawa kishahidi pamoja naye, wakachukuliwa wakina mama na watoto na kupelekwa Shama. Shekh Mufidi anasema: Msafara wa vichwa uliongozwa na Zuhar bun Qais akiambatana na Abu Barda bun Auf Al-Azadiy na Twariq bun Abu Dhabyaan wakiwa na jopo la watu wa Kufa, na msafara wa wanawake na watoto uliongozwa na Tha’alaba Aaidhiy na Shimri bun Thijaushen na Thabthu bun Rabii na Omari bun Hajjaaj wakiwa na wapanda farasi elfu moja. Na katika riwaya nyingine, wapanda farasi walikua elfu moja na mia tano, na inasemekana walikua elfu mbili au zaidi, miongoni mwao watu hamsini walikua ni walinzi wa kichwa kitakatifu (cha Imamu Hussein a.s).

Bibi Zainabu (a.s) akatembea safari yenye machungu makubwa, akiwa ametanguliwa na vichwa vya vipenzi wake huku kazungukwa na mayatima na wajane wakiwa juu ya migongo ya ngamia wasio kua na vikalio (vitandiko), wakati yeye ni mtoto wa mtu ambaye nafasi yake kwa Mtume (s.a.w.w) ni sawa na nafasi ya Haruna kwa Nabii Mussa (a.s), na mama yake ni mbora wa wanawake, alikua anatembea huku akiwa na maumivu makubwa, roho yake imejaa uchungu, nyota zimeondoka, jua limezama, miili mitakatifu imevuliwa pete na mapambo.

Safari iliendele… hadi wakafika mbali na jela la Kufa, wakaepukana na dhulma za bun Ziyadi.. wakiwa wanaenda Damaska, wanako subiriwa na Twaghuti.. Ahlulbait (a.s) walikua wanatembea wakiwa na subira kubwa huku roho zao zimejaa imani na uchamungu wakifahamu wazi kua anaye wapa mitihani anafahamu kua wanaweza kuihimili.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: