Sayyid Swafi atembelea majeruhi wa jeshi la serikali na Hashdi Sha’abi, na asisitiza kuwapa msaada unao endana na kujitolea kwao..

Maoni katika picha
Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmad Swafi (d.i) amesisitiza kuendelea kwapa huduma bora za kimatibabu majeruhi wa jeshi la serikali na wale wa Hashdi Sha’abi walio lazwa katika hospitali ya rufaa Alkafeel iliyo chini ya Ataba tukufu, akaahidi kuwapatia mahitaji ya kimatibabu katika ubora mkubwa kwa sababu ya kujitolea kwao katika kukomboa aridhi ya Iraq na maeneo matakatifu kutoka mikononi mwa magaidi ya Daesh.

Aliyasema hayo alipo watembelea hospitalini, ikiwa ni miongoni mwa ratiba ya kutembelea majeruhi wa jeshi la serikali na Hashdi Sha’abi waliopo katika hospitali ya rufaa Alkafeel au katika hospitali zingine. Katika ziara hii Sayyid Ahmadi Swafi alifuatana na mkuu wa hospitali hiyo dokta Haidari Bahadeli, aliye kua anampa maelezo kuhusu aina ya matibabu na huduma wanazo pewa majeruhi hao.

Mwishoni mwa ziara yao, kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu, alisifu ushujaa na ujasiri wa majemedari hao, akasema kua utukufu walionao haupatikani ispokua kwa watu ambao wameteuliwa na Mwenyezi Mungu kwa utukufu huo, akamuomba Mwenyezi Mungu awaponye haraka. Na akasifu madaktari na wauguzi namna wanavyo wahudumia na kuwataka waongeze juhudi zaidi.

Kumbuka kua uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, tangu kufunguliwa kwa hospitali hii iliweka vipao mbele vyake, miongoni mwa vipao mbele hivyo ni kutoa msaada wa matibabu kwa majemedari walio itikia fatwa tukufu ya kujilinda, na wakawa tayali kujitolea damu na uhai wao kwa ajili ya kulinda aridhi ya Iraq na maeneo matukufu yasinajisiwe na magaidi ya Daesh.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: