Televishen (Luninga) ya Hud-Hud yaonyesha azma ya kufungua chanel kwa kushirikiana na Maahadi ya Qur’an tukufu..

Maoni katika picha
Televishen ya Hud-Hud imeonshesha azma ya kufungua chanel kwa kushirikiana na Maahadi ya Qur’an tukufu ambayo ipo chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, chanel itakayo rusha matangazo yake kwa lugha tatu, (Kiarabu, Kiengereza na Kifarsi) na italenga ngazi muhimu ya umri wa mwanadamu kuanzia miaka 3 hadi 15 wa jinsia zote.

Hayo yalisemwa katika kikao baina ya mkuu wa televishen Ustadh Ihsaan Hilmiy na ugeni ulio wakilisha Maahadi ya Qur’an tukufu, ukiongozwa na mkuu wa Maahadi Shekh Jawaad Nasraawiy, aliye ambatana na chopo la wanafunzi wanaoshiriki katika mradi wa kiongozi wa wasomaji wa kitaifa unao endeshwa na Maahadi, kikao hicho kilifanyika makao makuu ya Televishen (Luninga) hiyo yaliyopo katika Jamhuri ya Iran.

Hilmiy alionyesha kua: “Yupo tayali kuanzisha program za Qur’an kwa kushirikiana na Maahadi ya Qur’an tukufu, miongoni mwa program hizo ni kutangaza vipaji vya wanafunzi wanao shiriki katika mradi wa kiongozi wa wasomaji wa kitaifa, kutokana na ushirikiano huo luninga ya Hud-Hud ya kiarabu itakua kama ya ki-iraq, na sisi tupo tayali kutumia kila aina ya uwezo wetu kufikisha sauti ya Qur’an na harakati zinazo fanywa na Maahadi katika kila sehemu ya dunia, Luninga hii inawatazamaji wengi kutoka nchi mbalimbali kote duniani”.

Mwishoni mwa mkutano wao, Hilmiy aliishukuru Atabatu Abbasiyya tukufu na idara ya Maahadi ya Qur’an kwa juhudi kubwa wanayo fanya kuhakikisha wanatengeneza kizazi kinacho itambua Qur’an na kushikamana na Ahlulbait (a.s).

Rais wa Ugeni huo Shekh Nasraawiy naye pia alishukuru kwa mapokezi mazuri waliyo pewa, na kwa kupewa fursa hii ambayo itakua sawa na muendelezo wa mazuri yanayo fanywa na luninga hii katika kutangaza tamaduni ya Qur’an na kuisimika kwa watu wa umri wanao ukusudia.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: