Wanahabari wa ki-iraq wametembelea Atabatu Abbasiyya tukufu asubuhi ya leo Juma Tano (20 Muharam 1439h) sawa na (11 Oktoba 2017m).
Wanahabari hao wametoka katika mikoa ya (Bagdad, Basra, Naswiriyya, Misaan, Baabil, Karbala na Najaf), baada ya kukamilisha ibada ya ziara katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), wametembelea makumbusho ya Alkafeel iliyo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, na wakaangalia vifaa kale vilivyomo ambavyo vinawakilisha zama tofauti za kihistoria.
Shekh Swaadiq Baswariy (Rais wa taasisi ya Ahlulbait) ambaye ndio kiongozi wa msafara huo ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Tumejikushanya wanahabari kutoka mikoa mbalimbali ili kuunda kundi maalumu na kuja kufanya ziara katika Atabatu Abbasiyya tukufu na kutembelea makumbusho yake ili tuone vifaa kale vilivyopo vyenye thamani kubwa na vinavyo wakilisha wakati mbalimbali wa kihistoria, baadhi ya vifaa historia yake inarudi maelfu ya miaka kabla ya kuzaliwa kwa Issa bun Maryam (b,d), hali kadhalika ni kwa ajili ya kuwatambulisha ndugu zangu ufanyaji kazi wa Atabatu Abbasiyya tukufu na kuhamisha uzoefu wake katika taasisi au nchi zingine kupitia vyombo vya habari”.
Akaongeza kusema kua: “Hakika vyombo vya habari vinamchango mkubwa sana katika kutangaza ukweli na kuufikisha kwa walengwa, kupitia vyombo vya habari tunaweza kufikisha ujumbe sahihi, tunaushukuru uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu na watumishi wake wote kwa mapokezi mazuri na tunawatakia mafanikio mema katika kazi zao kwa baraka ya Abulfadhil Abbasi (a.s)”.