Chini ya kauli mbiu (Imamu Hussein ametuunganisha) walimu na wanafunzi wa vyuo vya Iraq wamemuahidi na kuomboleza Abul-Ahraar Imamu Hussein (a.s) katika kumbukumbu ya kuuawa kwake, asubuhi ya Alkhamisi (20 Muharam 1439h) sawa na (12 Oktoba 2017m) wametoka wanafunzi zaidi ya 4000 na walimu zaidi ya 500, wakiwa katika makundi, kila kundi likiwa limebeba jina moja miongoni mwa majina ya watu waliouawa pamoja na Imamu Hussein (a.s), wakitanguliwa na bendera za taifa pamoja na bendera za maombolezo.
Matembezi hayo yalianzia katika barabara ya Kibla ya Abulfadhil Abbasi (a.s) wakaenda hadi katika ukumbi mtukufu wa haram, wakipitia eneo la katikati ya haram mbili tukufu, kisha wakaenda hadi katika kaburi la Imamu Hussein (a.s), wakahitimisha kwa kufanya majlis ya maombolezo, katika kauli zao wamesisitiza kufuata mwenendo wa Imamu Hussein (a.s) na kuenzi misingi yake.
Mkuu wa kituo cha harakati katika chuo kikuu cha Waasit Ustadh Muhammad Hamza Rabii amesema kua: “Kama kawaida yetu, leo tumetoka kwa pamoja katika matembezi ya maombolezo, tukiwa vyuo vikuu na Maahadi mbalimbali za Iraq, tukiwa watu wa tabaka na mitazamo tofauti ya dini, wote tumekusanyika chini ya bendera ya islahi iliyo pandishwa na Imamu Hussein (a.s) kwa watu wa tabaka zote wa Iraq, kupitia matembezi haya tunatuma ujumbe kwa walimwengu kua, hakika wananchi wa Iraq ni wamoja, hawatengani wala hawagawiki, huu ndio msimamo wa wanafunzi na walimu ambao wanaunda tabaka la watalamu katika jamii, na kupitia matembezi haya tunamuahidi Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), tutafuata mwenendo wao na tutabeba ujumbe wao mtukufu na kuutangaza duniani kote.