Kukamilika kwa maandalizi ya kushiriki katika kongamano la msimu wa Ashura..

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia kitengo cha habari na utamaduni imekamilisha maandalizi ya kushiriki katika kongamano la msimu wa Ashura linalo fanywa na Atabatu Husseiniyya tukufu katika mji wa Takaab huko Iran, kwa kushirikiana na taasisi mbili ya Jaan Nasharaan Abaa Abdillahi Hussein (a.s) na Razmankaan Islaam, litakalo fanyika tarehe (12-17 Oktoba 2017) sawa na (21-26 Muharam 1439h).

Ushiriki wa Atabatu Abbasiyya tukufu sambamba na Atabatu Husseiniyya na Kadhimiyya katika kongamano hili ni sehemu ya mpango wake wa kushiriki katika makongamano ya kimataifa, katika kongamano hili itawakilishwa na idara zitakazo onyesha vitu mbalimbali vya kitamaduni miongoni mwa vitu hivyo ni:

  • 1- Picha za Atabatu Abbasiyya tukufu na picha za wapiganaji wa Hashdi Sha’abi zinazo onyesha naomna walivyo itikia fatwa ya Marjaa dini mkuu.
  • 2- Picha zinazo onyesha namna Ataba za Karbala zilivyo shambuliwa wakati wa utawala wa zamani (Sadam) katika maandamano matukufu ya Shaabaniyya.
  • 3- Kugawa mikoba (folda) na zawadi kutoka katika Atabatu Abbasiyya tukufu.
  • 4- Kitengo kitakacho elezea tukio la twafu.

Kumbuka kua lengo la kufanyika kwa kongamano hili na kushiriki, ni kufikisha mazingira ya kiroho yaliyopo katika Ataba tukufu za Iraq katika nchi zingine duniani.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: