Atabatu Abbasiyya tukufu yapata mahudhurio ya aina yake katika maonyesho ya vitabu ya kimataifa..

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu –kama kawaida yake katika kila maonyesho- imepata mahudhurio makubwa katika ushiriki wake kwenye maonyesho ya visomo vya Sajadiyya (Taratiil Sajadiyya) vitabu ya kimataifa awamu ya nne, yanayo simamiwa na Atabatu Husseiniyya tukufu na kufanyika katika eneo la katikati ya haram mbili tukufu, yaliyo anza jana Alkhamisi (21 Muharam 1439h) sawa na (12 Oktoba 2017m) na yatachukua siku kumi, hii inatokana na vitu wanavyo onyesha kupitia matawi yao yanayo shiriki, ambayo yanatokana na kitengo cha habari na utamaduni pamoja na kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu, ambayo ni kazi nziri iliyo fanywa na wataalamu na waandishi wa vitengo hivyo, vitengo hivyo vinafanya kazi bega kwa bega pamoja na vituo na taasisi za usambazaji wa vitabu za kitaifa na kimataifa ambazo zinafika jumla ya taasisi (50).

Tawi la kitengo cha habari na utamaduni limeshiriki likiwa na machapicsho mengi ya vitabu vya kusomeshea, rejea na vitabu vingine mbalimbali, pia wana CD za aina mbalimbali, zenye mafundisho ya dini, Akhlaq na malezi pamoja na masomo ya kisekula, na kuna machapisho yaliyo tolewa katika muonekano mpya, pia yanalenga watu wa rika zote.

Nalo tawi la kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu, pia limeshiriki likiwa na machapisho yake mbalimbali pamoja na yale ya vituo vilivyo chini yake, kama vile kituo cha (turathi za Karbala, kituo cha turathi za Hilla na kituo cha turathi za Basra), pamoja na machapisho yanayo fanywa na kitengo hiki katika Maahadi ya Qur’an tukufu, ikiwa ni pamoja na chapisho la Qur’an tukufu iliyo chapishwa na Atabatu Abbasiyya.

Kiongozi wa maonyesho haya Ustadh Ali Ali amebainisha kua: “Hakika awamu hii ya maonyesho inakamilisha awamu zingine zilizo tangulia, na katika awamu hii vimeshiriki vituo (50) kutoka ndani na nje ya Iraq wakiwa na anuani za vitabu karibia (8000), upekee wa maonyesho ya mwaka huu, kuna vitabu vingi vinavyo elezea historia ya Imamu Sajaad (a.s), kuna aina za vitabu zaidi ya (55) vinavyo elezea historia yake, lengo la kufanya maonyesho haya ni kutangaza ujumbe wa Ahlulbait (a.s)”.

Kumbuka kua maonyesho ya visomo vya sajadiyya (Taratiil sajadiyya) ambayo ni sehemu muhimu ya maonyesho haya, yanafanyika kwa mara ya nne mfululizo, na lengo lake kuu ni kuangazia maisha ya Imamu Zainul-Abidina bun Hussein (a.s), hususan kukitangaza kitabu chake cha Risalatul Huquqi, kwa sababu kimesahaulika, sambamba na kukitangaza kitabu hicho huonyeshwa vitabu mbalimbali na vituo vya usambazaji wa vitabu vya kitaifa na kimataifa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: