Alasiri ya Ijumaa (22 Muharam 1439h) sawa na (13 Oktoba 2017m) limefanyika kongamano la kumi la mawakibu na vikundi vya Husseiniyya watakao shiriki katika ziara ya Arbainiyya mwaka huu, na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Ahmadi Swafi alitoa neno, miongoni mwa aliyo sema ni:
- 1- Maimamu (a.s) wamehimiza kuhuisha kumbukumbu ya msiba wa Imamu Hussein (a.s), na mashairi ni moja ya aina za uhuishaji huo, Imamu Swaadiq (a.s) alikua anapenda kuimbwe mashairi katika njia za Iraq kutokana na athari inayo patikana katika mashairi hayo.
- 2- Iraq imekua kinara katika ulimwengu wa mashairi ya huzuni, hakika mashairi hayo humliwaza muiraq na asiye kua muiraq, sawa yawe mashairi ya Qaridh au Daraaj, hakika tukio la Imamu Hussein Sayyid Shuhadaa (a.s) limeteka ulimwengu wa mashairi, na mashairi ya tukio la Twafu yana mvuto wa pekee.
- 3- Sisi tunajivunia nyie kutokana na namna mnavyo tilia umuhimu swala la mashairi katika mawakibu zenu.
- 4- Kuwepo kwa mawakibu Husseiniyya ni miongoni mwa hali zinazo ashiria kuwepo kwa kundi linalo pinga batili na dhulma, kwani kundi hilo linapambana na dhulma hata kama ikiwa wanao dhulumiwa sio wao, kwani wanafahamu sauti yeyote ya Imamu Hussein inamaanisha uadilifu.
- 5- sisi tumeishi katika zama ambazo ilikua haziruhusiwi harakati zozote za maombolezo ya msiba wa Imamu Hussein hapa Iraq, na walijitahidi kuondoa athari zote kuhusu Imamu Hussein, hadi kwenda kufanya ziara katika kaburi lake ilipigwa marufuku, na wakati mwingine watu waliojaribu kufanya maombolezo au kwenda kumzuri Imamu Hussein (a.s), walihukumiwa kufungwa jela ilichukuliwa kua ni jambo lisilofaa katika dini.
- 6- Sasa hivi tupo katika zama ambazo jamii inauwelewa mkubwa sana, na tuna mawakibu na vikundi vingi vya Husseiniyya vinavyo kataa dhulma.
- 7- Ziara ya Arbainiyya ni ya aina yake, mu-umin husafiri hadi katika kaburi la Sayyid Shuhadaa (a.s), na ujumbe anaobeba unahitaji msimamo imara.
- 8- Ziara ya Imamu Hussein (a.s) katika Arbainiyya inamazingira ya huzuni zaidi kushinda mwezi kumi Muharam, katika ziara hiyo; hukumbukwa huzuni na misukosuko aliyo pitia bibi Zainabu (a.s) akiwa pamoja na mateka pamoja na Imamu Sajaad (a.s) walipo kuja Karbala.
- 9- Mazingira ya Arbainiyya ndiyo tuliyo lelewa na kukulia, tumesimuliwa visa mbalimbali vya tukio la mauaji kutoka kwa washairi na wahadhiri, hakika mazingira ya Arbainiyya ni mazingira ya huzuni.
- 10- Pamoja na uwezo mkubwa aliokuanao Imamu Hussein (a.s) pamoja na maimamu wengine (a.s) lakini walionyesha huzuni kufuatia tukio la hili, Imamu Ridha (a.s) anasema: (Hakika siku (aliyo uawa) Hussein huvunja nguvu zetu na hututoa machozi na hudhalilika mtukufu wetu).
- 11- Swala la Imamu Hussein lina mazingatio na huzuni, jambo hili yapasa watu wa mawakibu walifahamu na kulizingatia katika kaswida zao na semi zao.
- 12- Tunatarajia wahudumu wa mawakibu wamfanye Imamu Hussein (a.s) kua kiigizo chao katika shughuli zao zote, ili wapate radhi za Mwenyezi Mungu pia na radhi ya Imamu Hussein (a.s).
- 13- Ni juu yenu enyi wahudumu wa mawakibu za Husseiniyya, mzipangilie maukibu zenu vizuri, hakika Imamu Hussein (a.s) alikua anapangilia shughuli zake katika ubora mkubwa tena nidhamu yake ilikua kubwa zaidi ya maelezo.
- 14- Wahudumu wa mawakibu wanatakiwa kuamiliana vizuri na watu wote wanaoratibu matembezi ya maombolezo pamoja na kulinda na kuhifadhi mali za watu.
- 15- Iraq ni nchi ya washairi bila upinzani, na mashairi yanayo elezea tukio la Imamu Hussein (a.s) yana nafasi kubwa sana, tunahitajia zaidi kaswida zenye vionjo vya huzuni.
- 16- Hakika juhudi zinazo fanywa na serikali ya Karbala na Ataba tukufu ni sehemu ya majukumu yao, tunatakiwa kusaidiana nao.
- 17- Ni lazima kuheshimu na kufuata maelekezo yanayo tolewa na kitengo cha minasabati na vikundi vya Husseiniyya yanayo lenga kupangilia na kuratibu utendaji.