Kongamano la msimu wa Ashura linalo simamiwa na Atabatu Husseiniyya tukufu katika mji wa Takab huko Iran, na kushiriki Atabatu Abbasiyya na Kadhimiyya tukufu, wamefanya mambo mbalimbali yanayo endana na mwezi wa huzuni kwa familia ya Mtume Muhammad (s.a.w.w), miongoni mwa mambo yaliyo fanyika katika siku ya pili ya kongamano hili ni kutoa muhadhara na kufanya kisomo cha Qur’an tukufu katika msikiti mkuu wa Shahristani katika mji huo.
Muhadhara ulitolewa na Shekh Swafaau Khazrajiy kutoka katika taasisi ya Daliil iliyo chini ya Atabatu Husseiniyya katika mji mtukufu wa Qum, alizungumzia kuishi kwa amani na usalama kuliko fundishwa na dini tukufu ya Uislamu, na yanayo fanywa na vikundi vya kigaidi na kitakfiri katika kuvunja misingi hii mitukufu ya kiislamu.
Kisomo cha Qur’an tukufu kilicho burudisha masikio ya wahudhuriaji kilisomwa na wafuatao: (Hussein Habibi kutoka Iran, Sajaad Ahmad kutoka katika Atabatu Kadhimiyya tukufu, Aaram Abdiy Zaadah kutoka katika mji mwenyeji wa kongamano, Muhammad Amiri Tamimi kutoka katika Atabatu Abbasiyya tukufu, Sayyid Mahdi Husseini kutoka katika Atabatu Husseiniyya tukufu na mwisho alikua ni Buya Ridhaaiy kutoka Iran).
Hafla ya Qur’an ilihitimishwa kwa kufanya majlis ya maombolezo ya Sayyid Shuhadaa Imamu Hussein (a.s), iliyo somwa na Shekh Abdulhussein Aakhund kutoka katika Atabatu Husseiniyya tukufu.
Program hizo zilipata mahudhurio makubwa sana kutoka kwa wakazi wa mji wa Takab na miji ya jirani, pamoja na ugeni unao wakilisha Ataba tukufu, Husseiniyya, Kadhimiyya na Abbasiyya.