Mtafiti dokta Yusufu Naswiriy kutoka katika kituo cha turathi za Karbala kilicho chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu amesisitiza kua; Harakati za Mawahabi hazina uhusiano wowote na moja ya madhehebu nne za kiislamu (kisunni), kutokana na utafiti alio zungumza katika nadwa ya kielimu iliyo endeshwa na Baitul Hikma kwa kushirikiana na kituo cha Markazi Wathaiqiy lidifai anil-muqadasaat na Markazi ya Ihyaau Turaath chini ya Ataba tukufu, utafiti alioupa jina lisemalo: (Mashambulio ya Mawahabi katika mji mtukufu wa Karbala).
Mtafiti huyu kazungumzia mashambulizi ya kigaidi yaliyo usibu mji mtukufu wa Karbala mwishoni mwa karne ya kumi na nane, baada ya kupatikana fikra za kiwahabi, ambazo zilileta hatari kubwa ulimwenguni, hususan katika nchi za kiarabu, amezungumzia jinai nyingi zilizo fanywa na kundi hili katika vita zao, ikiwa ni pamoja na mashambulizi waliyo fanya katika mji mtukufu wa Karbala bila kusahau uharibifu mkubwa walio fanya katika malalo mawili matakatifu (malalo ya Imamu Hussein na Abulfadhil Abbasi a.s) hii inaonyesha wazi kiwango kikubwa cha chuki walizo pandikizwa wafuasi wa kundi hilo.
Mzungumzaji wa pili ambaye pia ni mtafiti dokta Muhammad Ridha Hashimiy alibainisha kua: fikra za Kiwahabi kwa kiasi kikubwa sio sahihi, wanapotosha aya za Qur’an tukufu na hadithi za Mtume (s.a.w.w), na vyombo vya habari vya kitaifa na kimataifa vina mchango mkubwa katika kusambaza harakati zao.
Washiriki walitoa michango yao na kuuliza maswali, nao watoa mada walifafanua na kujibu maswali kama ilivyo hitajika.
Pembezoni mwa nadwa hii, kituo cha turathi za Karbala kilifanya maonyesho ya picha za aina mbili, aina ya kwanza zilikua mbao (16) zilizo kua na picha zinazo onyesha hatua mbalimbali ilizo pitia Atabatu Husseiniyya katika historia, na aina ya pili kulikua na picha (10) zinazo onyesha maandamano ya Shaabaniyya na uharibifu ulio fanywa wa kushambuliwa kwa Ataba mbili pamoja na mji mtukufu wa Karbala mwaka (1991) miladiyya.