Chini ya ushuhuda wa taasisi ya moyo ya Marekani, wataalamu wa kikundi cha uokoaji cha Alkafeel wahitimisha semina ya okoa uhai..

Maoni katika picha
Wataalamu wa Alkafeel katika mafunzo ya uokoaji vitani, miongoni mwa semina wanazo toa za uokozi (Okoa uhai kimsingi), ambapo wanafundisha namna ya kuokoa uhai wa majeruhi, na namna ya kufanya kazi katika mazingira magumu, semina hii iliandaliwa kwa ajili ya watumishi na wauguzi wa hospitali ya rufaa Alkafeel ambayo ipo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Semina hii imeshuhudiwa na kupasishwa na taasisi ya moyo ya Marekani, wamethibitisha kua; mafunzo yaliyo tolewa yamekidhi vigezo vya kimataifa vinavyo fatwa na taasisi hiyo, kutokana na walicho kiona, ambapo huhitajika uangalizi wa wakufunzi kwa wanafunzi na kuwaelekeza katika mambo ya kitaalamu.

Mafunzo hayo yaliyo chukua siku sita yalikua na washiriki (165), muda wote wa masomo ulikua saa (80), ambapo wamefundishwa namna ya kutambua mazingira hatari kwa haraka, na namna ya kutoa huduma ya kwanza na maelekezo yenye umakini mkubwa, pia wamefundishwa namna ya kutumia vifaa vya kupumulia, pamoja na mbinu mbalimbali za uokozi kwa watu wazima na watoto wadogo wanao nyoya.

Kumbuka kua wataalamu wa Alkafeel wanaofundisha uokozi (huduma ya kwanza) vitani, ambao wako chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, wamesha fundisha semina nyingi za aina hii zilizo husisha watu mbalimbali wakiwemo wapiganaji wa Hashdi Sha’abi na wamefaulisha mamia ya wanafunzi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: