Muhadhara wa kisekula katika siku ya tatu ya kongamano la msimu wa Ashura..

Maoni katika picha
Siku ya tatu ya wiki ya kongamano la kitamaduni linalo endelea katika mji wa Takab huko Iran (kongamano la msimu wa Ashura), linalo simamiwa na Atabatu Husseiniyya tukufu na kushiriki Atabatu Kadhimiyya na Abbasiyya, miongoni mwa ratiba zake ni muhadhara wa kisekula ulio wasilishwa asubuhi ya Juma Mosi (23 Muharam 1439h) sawa na (14 Oktoba 2017m) na Madrasa ya Rasul Akram (s.a.w.w) ya elimu za dini katika mji huo.

Anuani ya muhadhara huo ilikua inasema (Ubora wa dini ya kiislamu ukilinganisha na dini zingine) uliwasilishwa na dokta Ali Shekh kutoka chuo kikuu cha kimataifa cha Jaamiatul Mustwafa, akazungumzia vipengele muhimu ikiwa ni pamoja na mambo yenye utata yanayo nasibishwa na dini tukufu ya kiislamu.

Dokta Ali Shekh aliuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Kuna mambo mengi ambayo uwelewa wake hauko sahihi na kwa bahati mbaya tatizo hili ni kubwa sana katika jamii yetu ya kiislamu, kuna batili zimeingizwa katika uislamu mtukufu, kama vile uwelewa unaojengeka kua Uislamu ni dini ya uuaji na ubaguzi, kwa hiyo katika maelezo yangu nimejaribu kusahihisha uwelewa wa mafundisha sahihi ya uislamu, ili kuusafisha na tuhuma mbaya unazo pewa, kwa kutumia dalili za kiakili na kinakili kutoka ndani ya Qur’an tukufu na hadithi za Mtume (s.a.w.w) na Ahlulbait wake watakasifu (a.s)”.

Akaongeza kusema kua: “Hakika mada hizi zinaumuhimu mkubwa kwa ajili ya kurekebisha jamii yetu ya kiislamu hasa kundi la vijana linalo lengwa na fikra za chuki na ubaguzi, wanazo fundishwa na kuchochewa kua uislamu ni dini ya ubaguzi na mauaji, mambo ambayo kwa uhalisia hayapo kabisa katika dini tukufu ya kiislamu”.

Dokta Ali Shekh akahitimisha maelezo yake kwa kuzishukuru Ataba tukufu zilizo kuja kushiriki katika kongamano hili la msimu wa Ashura, kutokana na juhudi zao nzuri zinazo saidia kujenga maelewano baina ya watu, na kuondoa kila aina ya mifarakano, na moyo wao wa kuwasiliana na kila mfuasi wa Ahlulbaiti (a.s) kutoka sehemu zote za dunia.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: