Kundi la waombolezaji wa tukio la vita ya Karbala, lililo jumuisha wanafunzi na walimu wa chuo kikuu cha Karbala wamefanya matembezi ya maombolezo na kuonyesha uungaji wao mkono wa harakati ya Imamu Hussein (a.s).
Asubuhi ya Juma Pili (24 Muharam 1439h) sawa na (15 Oktoba 2017m), wanafunzi wa chuo kikuu cha Karbala walifanya matembezi ya maombolezo, yaliyo anzia barabara ya Abulfadhil Abbasi (a.s), wakatembeo hadi katika malalo yake (Abulfadhil Abbasi a.s) wakiwa wamebeba bendera na mabango, kisha wakatoka na kupitia katika eneo la katikati ya harm mbili, wakatembea hadi katika malalo ya Bwana wa Mashahidi Imamu Hussein (a.s), wakahitimisha kwa kufanya majlis ya maombolezo ndani ya ukumbi mtukufu wa haram ya Imamu Hussein (a.s), wakati wa matembezi walikua wanaimba kaswida za maombolezo zilizo onyesha ukubwa wa msiba, na kuahidi kufuata mwenendo wa haki ulioasisiwa na Bwana wa Mashahidi kwa damu yake takatifu, ambao imekua taa inayo waangazia wanaharakati wote ulimwenguni.
Kumbuka kua chuo kikuu cha Karbala hufanya maombolezo haya kila mwaka ndani ya mwezi huu wa huzuni, mwezi wa Muharam, ili kuonyesha kua; harakati ya Imamu Hussein (a.s) imeamsha tabaka la vijana wasomi na kuwapa shauku ya kufuata mwenendo wake mtukufu, ukizingatia kua wao ndio wanao unda jamii ya sasa na ya baadae.